sw_tn_fork/rev/14/08.md

21 lines
739 B
Markdown

# Umeanguka, umeanguka Babeli mkuu
Malaika anaizungumzia Babeli kuangamizwa kama vile imeanguka. "Babeli kuu imeangamizwa"
# Babebi kuu
"Babeli, ule mji mkuu" au "mji muhimu wa Babeli." Huu unawezekana kuwa ulikuwa ni alama ya mji wa Rumi ambao ulikuwa mkubwa, tajiri na wenye dhambi.
# uliwanywesha
Babeli inazungumziwa kana kwamba ni mtu badala ya mji uliojaa watu.
# kunywa divai ya tamaa zake mbaya
hii ni alama ya kushiriki katika tamaa zake mbaye za uasherati. "kuwa muasherati kama yeye" au "kulewa kama yeye na dhambi za uasherati"
# tamaa mbaya
Babeli inazungumziwa kama vile ni kahaba aliyesababisha watu wengine watende dhambi pamoja naye. Hii inaweza kuwa na maana mara mbili: uasherati halisi na pia kuabudu miungu.