# Umeanguka, umeanguka Babeli mkuu Malaika anaizungumzia Babeli kuangamizwa kama vile imeanguka. "Babeli kuu imeangamizwa" # Babebi kuu "Babeli, ule mji mkuu" au "mji muhimu wa Babeli." Huu unawezekana kuwa ulikuwa ni alama ya mji wa Rumi ambao ulikuwa mkubwa, tajiri na wenye dhambi. # uliwanywesha Babeli inazungumziwa kana kwamba ni mtu badala ya mji uliojaa watu. # kunywa divai ya tamaa zake mbaya hii ni alama ya kushiriki katika tamaa zake mbaye za uasherati. "kuwa muasherati kama yeye" au "kulewa kama yeye na dhambi za uasherati" # tamaa mbaya Babeli inazungumziwa kama vile ni kahaba aliyesababisha watu wengine watende dhambi pamoja naye. Hii inaweza kuwa na maana mara mbili: uasherati halisi na pia kuabudu miungu.