sw_tn_fork/psa/080/001.md

49 lines
1.1 KiB
Markdown

# Taarifa ya Jumla
Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania.
# Kwa mwanamuziki mkuu
"Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu"
# weka katika Shoshannimu
Hii inaweza kuwa inamaanisha mtindo wa muziki.
# Zaburi ya Asafu
"Hii nizaburi ambayo Asafu aliandika."
# Mchungaji wa Israeli
Asafu anamzungumzia Mungu kama yule anayeiongoza na kuilinda Israeli.
# wewe uliyemwongoza Yusufu kama kundi
"wewe unayewaongoza uzao wa Yusufu kana kwamba ni kundi la kondoo"
# Yusufu
Hapa Yusufu inamaanisha taifa la Israeli.
# wewe uketiye juu ya makerubi
Mfuniko wa sanduku la agano hekaluni, ishara ya kiti cha enzi ambapo Mungu aliitawala Israeli, ilikuwa imeunganishwa na makerubi ya dhahbu, moja kila upande, zikitazamana.
# ung'ae kwetu
Asafu anamzungumzia Mungu kana kwamba ni jua, linalotoa mwanga, sitiari ya unyofu. "tupe mwanga" au "tuoneshe njia sahihi ya kuishi"
# tikisa nguvu yako
Msemo "tikisa" inamaanisha "weka katika matendo"
# fanya uso wako ung'ae kwetu
Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwatendea kwa fadhila kana kwamba uso wa Yahwe uling'aa mwanga kwao.
# na tutaokoka
"na tafadhali tuokoe" au "ili utuokoe"