# Taarifa ya Jumla Usambamba ni kawaida katika mashairi ya Kiebrania. # Kwa mwanamuziki mkuu "Hii ni kwa kiongozi wa muziki kutumia katika kuabudu" # weka katika Shoshannimu Hii inaweza kuwa inamaanisha mtindo wa muziki. # Zaburi ya Asafu "Hii nizaburi ambayo Asafu aliandika." # Mchungaji wa Israeli Asafu anamzungumzia Mungu kama yule anayeiongoza na kuilinda Israeli. # wewe uliyemwongoza Yusufu kama kundi "wewe unayewaongoza uzao wa Yusufu kana kwamba ni kundi la kondoo" # Yusufu Hapa Yusufu inamaanisha taifa la Israeli. # wewe uketiye juu ya makerubi Mfuniko wa sanduku la agano hekaluni, ishara ya kiti cha enzi ambapo Mungu aliitawala Israeli, ilikuwa imeunganishwa na makerubi ya dhahbu, moja kila upande, zikitazamana. # ung'ae kwetu Asafu anamzungumzia Mungu kana kwamba ni jua, linalotoa mwanga, sitiari ya unyofu. "tupe mwanga" au "tuoneshe njia sahihi ya kuishi" # tikisa nguvu yako Msemo "tikisa" inamaanisha "weka katika matendo" # fanya uso wako ung'ae kwetu Mwandishi anamzungumzia Yahwe kuwatendea kwa fadhila kana kwamba uso wa Yahwe uling'aa mwanga kwao. # na tutaokoka "na tafadhali tuokoe" au "ili utuokoe"