2.4 KiB
Warumi 01 Maelezo ya Jumla
Muundo na upangiliaji
Mstari wa kwanza ni aina ya utangulizi. Watu katika eneo la kale la Mediterania mara nyingi walianza barua zao kwa njia hii. Wakati mwingine hii inaitwa "salamu."
Dhana maalum katika sura hii
Injili
Sura hii inaashiria yaliyomo katika Kitabu cha Warumi kuwa "Injili" (Warumi 1:2). Kitabo cha Warumi sio injili kama Mathayo, Marko, Luka na Yohana. lakini, sura za 1-8 zinawasilisha injili ya kibiblia: Wote wametenda dhambi. Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zetu. Alifufuliwa tena ili tuweze kuwa na maisha mapya ndani yake.
Matunda
Sura hii inatumia mfano ya matunda. Mfano wa matunda mara nyingi inahusu imani ya mtu inayozalisha matendo mema katika maisha yake. Katika sura hii, inahusu matokeo ya kazi ya Paulo kati ya Wakristo wa Kirumi. (See: [[rc:///tw/dict/bible/other/fruit]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/faith]] and rc://*/tw/dict/bible/kt/righteous)
Ushtakiwa wa Ujumla na Ghadhabu ya Mungu
Sura hii inaeleza kwamba hakuna mtu aliye na udhuru. Sisi sote tunajua kuhusu Mungu wa kweli, Yahweh, kutoka kwa viumbe vyake vilivyopo karibu na sisi. Kwa sababu ya dhambi zetu na asili yetu ya dhambi, kila mtu hakika anastahili ghadhabu ya Mungu. Ghadhabu hii ilidhihirishwa na Yesu akifa msalabani kwa wale wanaomwamini. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/believe]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/sin]])
Mifano muhimu ya matamshi katika sura hii
"Mungu aliwapa"
Wasomi wengi wanaona maneno "Mungu aliwaacha" na "Mungu aliwaacha kufuata" kama maneno muhimu ya kitheolojia. Kwa sababu hii, ni muhimu kutafsiri maneno haya yakionyesha Mungu kutokuwa mtendaji mkuu. Hapa Mungu anaruhusu tu watu kufuata tamaa zao wenyewe, yeye hawalazimishi. (See: rc://*/ta/man/translate/figs-activepassive)
Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii
Misemo na dhana ngumu
Sura hii ina mawazo mengi magumu ndani yake. Jinsi Paulo anavyoandika hufanya maneno mengi katika sura hii kuwa vigumu kutafsiri. Labda mtafsiri anahitaji kutumia UDB kuelewa maana ya maneno. Na inaweza kuwa muhimu zaidi kutafsiri maneno haya kwa uhuru. Baadhi ya maneno magumu yanajumuisha: "utiifu wa imani," "ninayemtumikia katika roho yangu," "kutoka kwa imani hadi imani" na "kubadilishana utukufu wa Mungu asiyeharibika kwa mfano wa mtu anayeharibika."
Links:
| >>