sw_tn/rom/front/intro.md

8.1 KiB

Utangulizi wa Warumi

Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla

Maelezo ya Kitabu cha Warumi

  1. Utangulizi (1:1-15)
  2. Uadilifu kwa imani katika Yesu Kristo (1:16-17)
  3. Watu wote wanahukumiwa kwa sababu ya dhambi (1:18-3:20)
  4. Uadilifu kupitia Yesu Kristo kwa imani kwake (3:21-4:25)
  5. Matunda ya Roho (5:1-11)
  6. Adamu na Kristo walinganishwa (5:12-21)
  7. uwa kama Kristo katika maisha haya (6:1-8:39)
  8. Mpango wa Mungu kwa Israeli (9:1-11:36)
  9. Ushauri wa manufaa kwa kuishi kama Wakristo (12:1-15:13)
  10. Hitimisho na salamu (15:14-16:27)

Nani aliandika Kitabu cha Warumi?

Mtume Paulo aliandika Kitabu cha Warumi. Paulo alitoka mji wa Tarso. Alikuwa anajulikana kama Sauli katika maisha yake ya awali. Kabla ya kuwa Mkristo, Paulo alikuwa Mfarisayo. Aliwatesa Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara kadhaa katika Ufalme wa Roma akiwaambia watu kuhusu Yesu.

Paulo huenda aliandika barua hii alipokuwa akiishi katika mji wa Korintho wakati wa safari yake ya tatu kwenye Ufalme wa Roma.

Je, kitabu cha Warumi kinahusu nini?

Paulo aliandika barua hii kwa Wakristo huko Roma. Paulo alitaka wawe tayari kumpokea wakati aliwatembelea. Alisema kusudi lake lilikuwa "kuleta utiifu wa imani" (16:26).

Katika barua hii Paulo alieleza kikamilifu Injili ya Yesu Kristo. Alielezea kuwa Wayahudi na Wayunani wamefanya dhambi, na Mungu atawasamehe na kuwaita wenye haki tu ikiwa wanaamini Yesu (sura ya 1-11). Kisha akawapa maelekezo ya manufaa kuhusu jinsi waumini wanapaswa kuishi (sura 12-16),

Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?

Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake asilia, "Warumi." Au wanaweza kuchagua kichwa kilicho wazi zaidi, kama "Barua ya Paulo kwa Kanisa la Roma," au "Barua kwa Wakristo huko Roma." (See: rc://*/ta/man/translate/translate-names)

Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za Kitamaduni

Je, ni majina yapi yanayotumiwa kumtaja Yesu?

Katika Warumi, Paulo alielezea Yesu Kristo kwa majina mengi na maelezo: Yesu Kristo (1:1), Ukoo wa Daudi (1:3), Mwana wa Mungu (1:4), Bwana Yesu Kristo (1:7) , Kristo Yesu (3:24), Dhabihu ya upatanisho (3:25), Yesu (3:26), Yesu Bwana wetu (4:24), Bwana wa Majeshi (9:29), Jiwe la Kujikwaa na Mwamba wa Kosa (9:33), Mwisho wa Sheria (10:4), Mkombozi (11:26), Bwana wa Wafu na Wanaoishi (14:9), na Shina la Yese (15:12).

Je, maneno ya kidini katika Warumi yanapaswa kutafsiriwaje?

Paulo anatumia maneno mengi ya kitheolojia ambayo haitumiwi katika injili nne. Kama Wakristo wa mapema walijifunza zaidi juu ya maana ya Yesu Kristo na ujumbe wake, walihitaji maneno na maelezo kwa mawazo mapya. Baadhi ya mifano ya maneno haya ni "kuhesabiwa haki" (5:1), "kazi za sheria" (3:20), "dhabihu ya upatanisho" (5:10), "ukombozi" (3:25), "utakaso" (6) : 19), na "mwili wa asili" (6: 6).

Kamusi ya "maneno muhimu" inaweza kuwasaidia watafsiri kuelewa baadhi ya maneno haya. (See: rc://*/ta/man/translate/figs-abstractnouns)

Maneno kama yale yaliyopewa hapo juu ni magumu kuelezea. Mara nyingi ni vigumu au haiwezekani kwa watafsiri kupata maneno sawa na hayo katika lugha zao wenyewe. Inaweza kusaidia kujua kwamba maneno yaliyo sawa na maneno haya hayahitajiki. Badala yake, watafsiri wanaweza kuunda misemo mifupi ili kuweza kuwasiliana mawazo haya. Kwa mfano, neno "injili" linaweza kutafsiriwa kama "habari njema juu ya Yesu Kristo."

Watafsiri pia wanapaswa kukumbuka kwamba baadhi ya maneno haya yana maana zaidi ya moja. Maana yatategemea jinsi mwandishi anatumia neno katika kifungu fulani. Kwa mfano, "haki" wakati mwingine ina maana kwamba mtu hutii sheria ya Mungu. Wakati mwingine, "haki" inamaanisha kwamba Yesu Kristo ametii kikamilifu sheria ya Mungu kwa niaba yetu.

Paulo alimaanisha nini aliposema "waliosalia" wa Israeli (11:5)?

Wazo la "mabaki" ni muhimu katika Agano la Kale na kwa Paulo. Waisraeli wengi walikuwa wameuawa au kutawanyika kati ya watu wengine wakati Waashuri na kisha Wababiloni walinyakua ardhi yao. Wayahudi wachache tu walibakia. Walijulikana kama "waliosalia."

Katika 11:1-9, Paulo anazungumzia waliosalia wengine. Hawa ni Wayahudi ambao Mungu aliwaokoa kwa sababu waliamini Yesu. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/remnant)

Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri

Paulo alimaanisha nini aliposema kwa kuwa "katika Kristo"?

Maneno "katika Kristo" na maneno kama hayo yapo katika 3:24; 6:11, 23; 8:1,2,39; 9:1; 12:5,17; 15:17; na 16:3,7,9,10. Paulo alitumia maneno haya kama mfano ili kuonyesha kwamba waumini Wakristo ni wa Yesu Kristo. Kuwa wa Kristo inamaanisha mwamini anaokolewa na hufanywa rafiki na Mungu. Muumini pia ameahidiwa kuishi na Mungu milele. Hata hivyo, wazo hili linaweza kuwa vigumu kuwakilisha katika lugha nyingi.

Misemo hii pia ina maana maalum ambazo hutegemea jinsi Paulo aliyotumia katika kifungu fulani. Kwa mfano, katika 3:24 ("ukombozi ulioko ndani ya Kristo Yesu"), Paulo alimaanisha kuokolewa kwetu "kwa sababu" ya Yesu Kristo. Katika 8:9 ("ninyi hamko katika mwili bali katika Roho"), Paulo alizungumza juu ya waumini wanaomtii Roho Mtakatifu. Katika 9:1 ("Ninasema ukweli katika Kristo"), Paulo alimaanisha kuwa anasema ukweli ambao "unakubaliana na" Yesu Kristo.

Hata hivyo, wazo la msingi la sisi kuwa kwa umoja na Yesu Kristo (na kwa Roho Mtakatifu) linaoneka katika vifungu hivi pia. Kwa hiyo, mtafsiri ana uhuru wa kuchagua katika vifungu vingi vinavyotumia "ndani." Mara nyingi huamua kutumia maana ya karibu sana ya "ndani," kama, "kwa njia ya," "kwa namna ya," au "kuhusiana na." Lakini, ikiwa inawezekana, mtafsiri anapaswa kuchagua neno au maneno ambayo yanaelezea maana ya karibu sana na maana ya "umoja na." (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/inchrist)

Je, namuna gani mawazo ya "takatifu," "watakatifu" au "walio watakatifu," na "kutakasa" yanawakilishwa katika Warumi katika ULB?

Maandiko hutumia maneno kama hayo ili kuelezea moja kati ya mawazo mbalimbali. Kwa sababu hii, mara nyingi ni vigumu kwa watafsiri kuyawakilisha vizuri katika matoleo yao. Katika kutafsiri kwa Kiingereza, ULB inatumia kanuni zifuatazo:

  • Wakati mwingine maana yake katika kifungu inaashiria utakatifu wa maadili. Ya muhimu hasa katika kuelewa injili, ni ukweli kwamba Mungu anaona Wakristo kuwa wasio na dhambi kwa sababu wameungana na Yesu Kristo. Ukweli mwingine unaohusiana kwa karibu ni kwamba Mungu ni mkamilifu na hana hatia. Ukweli wa tatu ni kwamba Wakristo wanapaswa kuishi kwa njia isiyo na hatia wala doa katika maisha yao. Katika nyakati hizi, ULB inatumia "takatifu," "Mungu mtakatifu," "watakatifu" au "watu watakatifu." (Angalia: 1:7)
  • Wakati mwingine maana yake katika kifungu inaashiria Wakristo tu wala sio jukumu fulani wanalopaswa kufanya. Nyakati ambapo matoleo mengine ya Kiingereza yanatumia "watakatifu" au "walio watakatifu," ULB inatumia "waumini." (Angalia: 8:27; 12:13; 15:25, 26, 31; 16:2, 15)
  • Wakati mwingine maana yake katika kifungu inaonyesha wazo la mtu au kitu kilichotengwa ili kutumiwa na Mungu pekee. Katika matukio haya, ULB inatumia "kuwekwa pembeni," "kujitolea," "takaswa," au "iliyohifadhiwa." (Angalia: 15:16)

UDB mara nyingi husaidia ikiwa watafsiri wanawaza jinsi ya kuwakilisha mawazo haya katika tafsiri za lugha zao.

Je, ni yapi masuala makuu katika maandishi ya Kitabu cha Warumi?

Yafuatayo ni masuala ya muhimu zaidi katika Kitabu cha Warumi:

  • "[Mungu] hufanya vitu vyote kwa ajili ya mema" (8:28). Baadhi ya matoleo ya zamani husema, "Vitu vyote vinafanya kazi pamoja kwa kuvifanikisha."
  • "Lakini ikiwa ni kwa neema, si kwa sababu ya matendo tena, la sivyo neema haiwezi kuwa neema" (11:6). Nakala bora za kale zilisoma hivi. Hata hivyo, baadhi ya matoleo yasoma: "Lakini ikiwa ni kwa matendo, basi sio neema tena: la sivyo matendo hawezi tena kuwa matendo."
  • "Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe pamoja nanyi nyote. Amina." (16:24). Nakala bora za kale hazina aya hii.

Watafsiri wanashauriwa kutotafsiri kifungu hiki. Hata hivyo, ikiwa katika eneo la watafsiri, kuna matoleo ya zamani ya Biblia ambayo yanajumuisha kifungu hiki, watafsiri wanaweza kuijumuisha. Ikiwa zinatafsiriwa, zinapaswa kuwekwa ndani ya mabano ya mraba ([]) ili kuonyesha kwamba labda asili yao sio Kitabu cha Warumi. (See: rc://*/ta/man/jit/translate-textvariants)

(See: rc://*/ta/man/jit/translate-textvariants)