Mwandishi anajitambulisha kama Yuda nduguye Yakobo. Yuda na Yakobo walikuwa ndugu wa kambo wa Yesu Kristo. Haijulikani iwapo barua hii ilipaswa kuwa ya kanisa fulani.
Yuda aliaandika barua hii kuwaonya waumini kuhusu walimu wa uongo.Yuda alinukuu mara nyingi kutoka Agano la Kale. Hii inaweza ashiria kwamba Yuda aliandikia hadhira ya Wakristo wa Kiyahudi. Barua hii na 2 Petero zina ujumbe wenye kufanana. Barua zote zinazungumzia malaika, Sodoma na Gomorah na walimu wa uongo.
### Kichwa cha kitabu hiki kitafsiriwe namna gani?
Watafsiri wanaweza kuchagua kukiita kitabu hiki kutumia kichwa chake cha kitamaduni, "Yuda." ama wanaweza chagua kichwa kinachoeleweka zaidi kama "Barua kutoka kwa Yuda" ama "Barua aliyoandika Yuda." (Tazama: [[rc://*/ta/man/translate/translate-names]])
Kuna uwezekano Yuda aliwakemea watu watajulikana kwa jina Wagnostiki. Walimu hawa waliharibu mafundisho ya maandiko matakatifu kwa manufaa yao wenyewe. Waliishi maisha maovu na wakafundisha watu kuishi hivyo .