# Utangulizi wa Yuda ## Sehemu ya 1 Maelezo ya Jumla ### Muhtasari wa kitabu cha Yuda 1. Utangulizi (1:1-2) 1. Onyo kuhusu walimu wa uongo (1:3-4) 1. Mifano ya Agano la Kale(1:5-16) 1. Jibu linalostahili (1:17-23) 1. Utukufu kwa Mungu (1:24-25) ### Nani aliandika kitabu cha Yuda? Mwandishi anajitambulisha kama Yuda nduguye Yakobo. Yuda na Yakobo walikuwa ndugu wa kambo wa Yesu Kristo. Haijulikani iwapo barua hii ilipaswa kuwa ya kanisa fulani. ### Kitabu cha Yuda kinahusu nini? Yuda aliaandika barua hii kuwaonya waumini kuhusu walimu wa uongo.Yuda alinukuu mara nyingi kutoka Agano la Kale. Hii inaweza ashiria kwamba Yuda aliandikia hadhira ya Wakristo wa Kiyahudi. Barua hii na 2 Petero zina ujumbe wenye kufanana. Barua zote zinazungumzia malaika, Sodoma na Gomorah na walimu wa uongo. ### Kichwa cha kitabu hiki kitafsiriwe namna gani? Watafsiri wanaweza kuchagua kukiita kitabu hiki kutumia kichwa chake cha kitamaduni, "Yuda." ama wanaweza chagua kichwa kinachoeleweka zaidi kama "Barua kutoka kwa Yuda" ama "Barua aliyoandika Yuda." (Tazama: [[rc://*/ta/man/translate/translate-names]]) ## Sehemu ya 2: Dhana muhimu za kidini na kitamaduni. ### Ni watu gani Yuda aliwakemea? Kuna uwezekano Yuda aliwakemea watu watajulikana kwa jina Wagnostiki. Walimu hawa waliharibu mafundisho ya maandiko matakatifu kwa manufaa yao wenyewe. Waliishi maisha maovu na wakafundisha watu kuishi hivyo .