Thu Mar 17 2022 09:29:48 GMT+0200 (South Africa Standard Time)

This commit is contained in:
Tomussone José Machinga 2022-03-17 09:29:51 +02:00
commit 1dfd0b9271
434 changed files with 500 additions and 0 deletions

1
01/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Kitabu cha ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi, mwana wa Ibrahimu. \v 2 Ibrahimu alikuwa baba wa Isaka, na Isaka baba wa Yakobo, na Yakobo baba wa Yuda na ndugu zake. \v 3 Yuda alikuwa baba wa Peresi na Sera kwa Tamari, Peresi baba wa Hezeroni, na Hezeroni baba wa Ramu.

1
01/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 Ramu alikuwa baba wa Aminadabu, Aminadabu baba wa Nashoni, na Nashoni baba wa Salimoni. \v 5 Salimoni alikuwa baba wa Boazi kwa Rahabu, Boazi baba wa Obedi kwa Ruth, Obedi baba wa Yese, \v 6 Yese alikuwa baba wa mfalme Daudi. Daudi alikuwa baba wa Sulemani kwa mke wa Uria.

1
01/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Sulemani alikuwa baba wa Rehoboamu, Rehoboamu baba wa Abiya, Abiya baba wa Asa. \v 8 Asa alikuwa baba wa Yehoshafati, Yehoshafati baba wa Yoramu, na Yoramu baba wa Uzia.

1
01/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Uzia alikuwa baba wa Yothamu, Yothamu baba wa Ahazi, Ahazi baba wa Hezekia. \v 10 Hezekia alikuwa baba wa Manase, Manase baba wa Amoni na Amoni baba wa Yosia. \v 11 Yosia alikuwa baba wa Yekonia na kaka zake wakati wa kuchukuliwa kwenda Babeli.

1
01/12.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 12 Na baada ya kuchukuliwa kwenda Babeli, Yekonia alikuwa baba wa Shatieli, Shatieli alikuwa babu yake na Zerubabeli. \v 13 Zerubabeli alikuwa baba wa Abiudi, Abiudi baba wa Eliakimu, na Eliakimu baba wa Azori. \v 14 Azori alikuwa baba wa Zadoki, Zadoki baba wa Akimu, na Akimu baba wa Eliudi.

1
01/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Eliudi alikuwa baba wa Elieza, Elieza baba wa Matani na Matani baba wa Yakobo. \v 16 Yakobo alikuwa baba wa Yusufu mume wa Mariamu, ambaye kwa yeye Yesu alizaliwa, aitwaye Kristo. \v 17 Vizazi vyote tangu Ibrahimu hadi Daudi vilikuwa vizazi kumi na vinne, kutoka Daudi hadi kuchukuliwa kwenda Babeli vizazi kumi na vinne, na kutoka kuchukuliwa kwenda Babeli hadi Kristo vizazi kumi na vinne.

1
01/18.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 18 Kuzaliwa kwa Yesu Kristo kulikuwa kwa namna hii. Mama yake, Mariamu, alichumbiwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana, alionekana kuwa na mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. \v 19 Mume wake Yusufu, alikuwa mtu mwenye haki hakutaka kumwaibisha hadharani. Aliamua kusitisha uchumba wake naye kwa siri.

1
01/20.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 20 Alipokuwa akifikiri juu ya mambo haya, Malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akisema,'' Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu kama mkeo, kwa sababu mimba aliyonayo ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu. \v 21 Atajifungua mtoto wa kiume na utamwita jina lake Yesu, kwa maana atawaokoa watu wake na dhambi zao.''

1
01/22.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 22 Yote haya yalitokea kutimizwa kile kilichonenwa na Bwana kwa njia ya nabii, akisema, \v 23 "Tazama, bikira atachukua mimba na kuzaa mtoto wa kiume, na watamwita jina lake Imanueli"-- maana yake, "Mungu pamoja nasi."

1
01/24.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 24 Yusufu aliamka kutoka usingizini na kufanya kama malaika wa Bwana alivyomwamuru na alimchukua kama mkewe. \v 25 Hata hivyo, hakulala naye mpaka alipojifungua mtoto wa kiume na alimwita jina lake Yesu.

1
02/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Baada ya Yesu kuzaliwa katika Bethelehem ya Uyahudi katika siku za mfalme Herode, watu wasomi kutoka mashariki ya mbali walifika Yerusalemu wakisema, \v 2 "Yuko wapi yeye ambaye aliyezaliwa Mfalme wa Wayahudi? Tuliiona nyota yake mashariki nasi tumekuja kumwabudu." \v 3 Pindi Mfalme herode aliposikia haya alifadhaika, na Yerusalemu yote pamoja naye.

1
02/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 Herode akawakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, naye akawauliza, "Kristo atazaliwa wapi?" \v 5 Wakamwabia, "Katika Bethelehemu ya Uyahudi, kwa kuwa hivi ndivyo ilivyoandikwa na nabii, \v 6 Nawe Bethelehemu, katika nchi ya Yuda, si mdogo miongoni mwa viongozi wa Yuda, kwa kuwa kutoka kwako atakuja mtawala atakayewachunga watu wangu Israeli."

1
02/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Hivyo Herode aliwaita wale wasomi kwa siri na kuwauliza ni wakati gani hasa nyota ilikuwa imeonekana. \v 8 Akawatuma Bethelehem, akisema, "Nendeni kwa uangalifu mkamtafute mtoto aliyezaliwa. Wakati mtakapomwona, nileteeni habari ili kwamba mimi pia niweze kuja na kumwabudu."

1
02/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Baada ya kuwa wamemsikia mfalme, waliendelea na safari yao, na nyota ile waliyokuwa wameiona mashariki iliwatangulia hadi iliposimama juu ya mahali mtoto aliyezaliwa alipokuwa. \v 10 Wakati walipoiona nyota, walifurahi kwa furaha kuu mno.

1
02/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Waliingia nyumbani na kumuona mtoto aliyezaliwa na Mariamu mama yake. Walimsujudia na kumwabudu. Walifungua hazina zao na kumtolea zawadi za dhahabu, uvumba, na manemane. \v 12 Mungu aliwaonya katika ndoto wasirudi kwa Herode, hivyo, waliondoka kurudi katika nchi yao kwa njia nyingine.

1
02/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Baada ya kuwa wameondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto na kusema, "Inuka, mchukue mtoto na mama yake na mkimbilie Misri. Bakini huko mpaka nitakapowaambia, kwa kuwa Herode atamtafuta mtoto ili amwangamize. \v 14 Usiku huo Yusufu aliamka na kumchukua mtoto na mama yake na kukimbilia Misri. \v 15 Aliishi huko hadi Herode alipo kufa. Hii ilitimiza kile Bwana alichokuwa amenena kupitia nabii, "Kutoka Misri nimemwita mwanangu."

1
02/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Kisha Herode, alipoona kuwa amedhihakiwa na watu wasomi, alikasirika sana. Aliagiza kuuawa kwa watoto wote wa kiume waliokuwa Bethelehemu na wote katika eneo lile ambao walikuwa na umri wa miaka miwili na chini yake kulingana na wakati aliokuwa amekwisha thibitisha kabisa kutoka kwa wale watu wasomi.

1
02/17.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 17 Ndipo lilipotimizwa lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Yeremia, \v 18 "Sauti ilisikika Ramah, kilio na maombolezo makubwa, Raheli akiwalilia watoto wake, na alikataa kufarijiwa, kwa sababu hawapo tena."

1
02/19.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 19 Herode alipo kufa, tazama malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri na kusema, \v 20 "Inuka mchukue mtoto na mama yake, na mwende katika nchi ya Israeli kwa maana waliokuwa wakitafuta uhai wa mtoto wamekufa." \v 21 Yusufu aliinuka, akamchukua mtoto pamoja na mama yake, na wakaja katika nchi ya Israeli.

1
02/22.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 22 Lakini aliposikia kuwa Arikelau alikuwa anatawala Yuda mahali pa baba yake Herode, aliogopa kwenda huko. Baada ya Mungu kumuonya katika ndoto, aliondoka kwenda mkoa wa Galilaya \v 23 na alienda kuishi katika mji uitwao Nazareti. Hili lilitimiza kile kilichokuwa kimekwisha kunenwa kwa njia ya manabii, kwamba ataitwa Mnazareti.

1
03/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Katika siku zile Yohana Mbatizaji alikuja akihubiri katika nyika ya Yuda akisema, \v 2 "Tubuni kwa maana ufalme wa mbinguni u karibu." \v 3 Kwa maana huyu ndiye aliyenenwa na nabii Isaya akisema, "sauti ya mtu aitaye kutoka jangwani; 'wekeni tayari njia ya Bwana, yanyoosheni mapito yake."'

1
03/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 Sasa Yohana alivaa manyoya ya ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Chakula chake kilikuwa nzige na asali ya mwituni. \v 5 Kisha Yerusalemu, Yuda yote, na eneo lote linalozunguka mto Yorodani wakaenda kwake. \v 6 Walikuwa wakibatizwa naye katika mto Yorodani huku wakitubu dhambi zao.

1
03/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Lakini alipowaona wengi wa mafarisayo na masadukayo wakija kwake kubatizwa, akawaambia, ''Enyi uzao wa nyoka wenye sumu nani aliye waonya kuikimbia ghadhabu inayokuja? \v 8 Zaeni matunda yaipasayo toba. \v 9 Na msifikiri na kusemezana miongoni mwenu, 'Tunaye Ibrahimu kama baba yetu.' Kwa kuwa nawaambieni Mungu anaweza kumwinulia Ibrahimu watoto hata kutoka katika mawe haya.

1
03/10.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 10 Tayari shoka limekwisha kuwekwa kwenye mzizi wa miti. Kwahiyo kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa kwenye moto. \v 11 Ninawabatiza kwa maji kwa ajili ya toba. Lakini yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi nami sistahili hata kubeba viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. \v 12 Na pepeto lake li mkononi mwake kusafisha kabisa uwanda wake na kuikusanya ngano yake ghalani. Lakini atayachoma makapi kwa moto ambao hauwezi kuzimika.

1
03/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka mto Yorodani kubatizwa na Yohana. \v 14 Lakini Yohana alitaka kumzuia akisema, "Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?'' \v 15 Yesu akajibu akasema, ''Ruhusu iwe hivi sasa, kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.'' Kisha Yohana akamruhusu.

1
03/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Baada ya kuwa amebatizwa, mara Yesu alitoka kwenye maji, na tazama, Mbingu zikafunguka kwake. Na alimuona Roho wa Mungu akishuka kwa mfano wa njiwa na kutulia juu yake. \v 17 Tazama, sauti ilitoka mbinguni ikisema, "Huyu ni mwanangu mpendwa. Ninaye pendezwa sana naye.''

1
04/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Kisha Yesu aliongozwa na Roho mpaka jangwani ili ajaribiwe na ibilisi. \v 2 Alipokuwa amefunga kwa siku arobaini mchana na usiku alipata njaa. \v 3 Mjarabu akaja na akamwambia, "Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mkate." \v 4 Lakini Yesu alimjibu na kumwambia, "Imeandikwa, 'Mtu hataishi kwa mkate peke yake, bali kwa kila neno litokalo kinywani mwa Mungu.'''

1
04/05.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 5 Kisha ibilisi akampeleka katika mji mtakatifu na kumweka mahali pa juu sana pa jengo la hekalu, \v 6 na kumwambia,'' kama wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe chini, kwa maana imeandikwa, 'Ataamuru malaika wake waje wakudake,' na, 'watakuinua kwa mikono yao, ili usijikwae mguu wako katika jiwe."

1
04/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Yesu akamwambia, ''Tena imeandikwa, 'Usimjaribu Bwana Mungu wako.''' \v 8 Kisha, ibilisi akamchukua na kumpeleka sehemu ya juu zaidi akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari ya hizo zote. \v 9 Akamwambia, "Nitakupa vitu vyote hivi ukunisujudia na kuniabudu."

1
04/10.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 10 Kisha Yesu akamwambia, "Nenda zako utoke hapa, Shetani! Kwa maana imeandikwa, 'Yakupasa kumwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.'" \v 11 Kisha ibilisi akamwacha, na tazama, malaika wakaja wakamtumikia.

1
04/12.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 12 Basi Yesu aliposikia kuwa Yohana amekamatwa, aliondoka mpaka Galilaya. \v 13 Aliondoka Nazareti alienda na kuishi Kaperanaumu, iliyoko kandokando na Bahari ya Galilaya, mipakani mwa majimbo ya Zabuloni na Naftali.

1
04/14.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 14 Hii ilitokea kutimiza kile kilichonenwa na nabii Isaya, \v 15 "Katika mji wa Zabuloni na mji wa Naftali, kuelekea Baharini, ng'ambo ya Yorodani, Galilaya ya wamataifa! \v 16 Watu walio kaa gizani wameuona mwanga mkuu, na wale waliokuwa wameketi katika maeneo na kivuli cha mauti, juu yao nuru imewaangazia.''

1
04/17.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 17 Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri na kusema, "Tubuni, kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.''

1
04/18.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 18 Alipokuwa akitembea kandokando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni aliyekuwa akiitwa Petro, na Andrea kaka yake, wakitega nyavu baharini, kwa kuwa walikuwa wavuvi wa samaki. \v 19 Yesu akawaambia, "Njooni mnifuate, nitawafanya kuwa wavuvi wa watu." \v 20 Mara moja waliziacha nyavu na walimfuata.

1
04/21.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 21 Na Yesu alipokuwa akiendelea kutoka hapo aliwaona ndugu wawili wengine, Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana kaka yake. Walikuwa katika mtumbwi pamoja na Zebedayo baba yao wakishona nyavu zao. Akawaita, \v 22 na mara moja wakaacha mtumbwi na baba yao nao wakamfuata.

1
04/23.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 23 Yesu alienda karibia Galilaya yote, akifundisha katika Masinagogi yao, akihubiri injili ya ufalme, na akiponya kila aina ya maradhi na magonjwa miongoni mwa watu. \v 24 Habari zake zilienea Siria yote, na watu wakawaleta kwake wale wote waliokuwa wakiugua, wakiwa na maradhi mbalimbali na maumivu, waliokuwa na mapepo, na wenye kifafa na waliopooza. Yesu aliwaponya. \v 25 Umati mkubwa wa watu ulimfuata kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu na Uyahuda na kutoka ng'ambo ya Yorodani.

1
05/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Yesu alipo uona umati, akaondoka na kuelekea Mlimani. Alipokuwa ameketi chini, wanafunzi wake wakaja kwake. \v 2 Akafunua kinywa chake na akawafundisha, akisema, \v 3 "Heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao. \v 4 Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.

1
05/05.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 5 Heri wenye upole, maana watairithi nchi. \v 6 Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa. \v 7 Heri wenye rehema maana hao watapata Rehema. \v 8 Heri wenye moyo safi maana watamwona Mungu.

1
05/09.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 9 Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu. \v 10 Heri wale wanaoteswa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao.

1
05/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Heri ninyi ambao watu watawatukana na kuwatesa, au kusema kila aina ya ubaya dhidi yenu kwa uongo kwa ajili yangu. \v 12 Furahini na kushangilia, maana thawabu yenu ni kubwa juu mbinguni. Kwa kuwa hivi ndivyo watu walivyo watesa manabii walioishi kabla yenu.

1
05/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Ninyi ni chumvi ya dunia. Lakini kama chumvi imepoteza ladha yake, itawezaje kufanyika chumvi halisi tena? Kamwe haiwezi kuwa nzuri kwa kitu kingine chochote tena, isipokuwa ni kutupwa nje na kukanyagwa na miguu ya watu. \v 14 Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojegwa juu ya mlima haufichiki.

1
05/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Wala watu hawawashi taa na kuweka chini ya kikapu, bali kwenye kinara, nayo yawaangaza wote walio ndani ya nyumba. \v 16 Acha nuru yenu iangaze mbele za watu kwa namna ambayo kwamba, wayaone matendo yenu mema na kumtukuza Baba yenu aliye mbinguni.

1
05/17.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 17 Msifikiri nimekuja kuiharibu sheria wala manabii. Sijaja kuharibu lakini kutimiza. \v 18 Kwa kweli nawaambia kwamba mpaka mbingu na dunia zote zipite hapana yodi moja wala nukta moja ya sheria itaondoshwa katika sheria hadi hapo kila kitu kitakapokuwa kimekwisha timizwa.

1
05/19.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 19 Hivyo yeyote avunjaye amri ndogo mojawapo ya amri hizi na kuwafundisha wengine kufanya hivyo ataitwa mdogo katika ufalme wa mbinguni. Lakini yeyote azishikaye na kuzifundisha ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni. \v 20 Kwa maana nawaambia haki yenu isipozidi haki ya waandishi na Mafarisayo, kwa vyovyote vile hamtaingia katika ufalme wa mbinguni.

1
05/21.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 21 Mmesikia ilinenwa zamani kuwa, "usiue" na 'yeyote auaye yuko katika hatari ya hukumu.' \v 22 Lakini nawaambia yeyote amchukiaye ndugu yake atakuwa katika hatari ya hukumu. Na yeyote amwambiaye ndugu yake kuwa, 'Wewe ni mtu usiyefaa!' atakuwa katika hatari ya baraza. Na yeyote asemaye, 'Wewe mjinga!' atakuwa katika hatari ya moto wa jehanamu.

1
05/23.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 23 Hivyo kama unatoa sadaka yako katika madhabahu na unakumbuka kuwa ndugu yako ana jambo lolote dhidi yako, \v 24 iache sadaka mbele ya madhabahu, kisha shika njia yako. Kapatane kwanza na ndugu yako, na kisha uje kuitoa sadaka yako.

1
05/25.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 25 Patana na mshitaki wako upesi, ukiwa pamoja naye njiani kuelekea mahakamani, vinginevyo mshtaki wako anaweza kukuacha mikononi mwa hakimu, na hakimu akuache mikononi mwa askari, nawe utatupwa gerezani. \v 26 Amini nawaambieni, kamwe hutawekwa huru hadi umelipa senti ya mwisho ya pesa unayodaiwa.

1
05/27.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 27 Mmesikia imenenwa kuwa, 'Usizini.' \v 28 Lakini nawaambieni yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake.

1
05/29.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 29 Na kama jicho lako la kulia linakusababisha kujikwaa, ling'oe na ulitupe mbali nawe. Kwa kuwa ni afadhali kiungo kimoja katika mwili wako kiharibike kuliko mwili mzima kutupwa jehanamu. \v 30 Na kama mkono wako wa kuume unakusababisha kujikwaa, ukate kisha uutupilie mbali nawe. Maana ni afadhali kiungo kimoja katika mwili wako kiharibike kuliko mwili mzima kutupwa jehanamu.

1
05/31.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 31 Imenenwa pia, yeyote amfukuzaye mkewe, na ampe hati ya talaka.' \v 32 Lakini mimi nawaambia, yeyote anaye mwacha mke wake, isipokuwa kwa kwa sababu ya zinaa, amfanya kuwa mzinzi. Na yeyote amuoaye baada ya kupewa talaka afanya uzinzi.

1
05/33.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 33 Tena, mmesikia ilinenwa kwa wale wa zamani, 'Msiape kwa uongo, bali pelekeni viapo vyenu kwa Bwana.' \v 34 Lakini nawaambia, msiape hata kidogo, ama kwa mbingu, kwa sababu ni enzi ya Mungu; \v 35 wala kwa dunia, maana ni mahali pa kuweka kiti cha kukanyagia nyayo zake, ama kwa Jerusalemu, maana ni mji wa mfalme mkuu.

1
05/36.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 36 Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. \v 37 Bali maneno yenu yawe, 'Ndiyo, ndiyo, Hapana, hapana.' Kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.

1
05/38.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 38 Mmesikia imenenwa kuwa, 'Jicho kwa jicho, na jino kwa jino.' \v 39 Lakini mimi namwambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na jingine pia.

1
05/40.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 40 Na kama yeyote anatamani kwenda na wewe mahakamani na akakunyang'anya kanzu yako, mwachie na joho lako pia. \v 41 Na yeyote akulazimishaye kwenda naye maili moja, nenda naye maili mbili. \v 42 Kwa yeyote akuombaye mpatie, na usimwepuke yeyote anayehitaji kukukopa.

1
05/43.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 43 Mmesikia imenenwa, 'Umpende jirani yako, na umchukie adui yako.' \v 44 Lakini nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanao waudhi, \v 45 Ili kwamba muwe watoto wa baba yenu aliye mbinguni. Kwa kuwa anafanya jua liwaangazie wabaya na wema, na anawanyeshea mvua waovu na wema.

1
05/46.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 46 Kama mkiwapenda wanaowapenda ninyi, mwapata thawabu gani? Kwani watoza ushuru hawafanyi hivyo? \v 47 Na kama mkiwasalimia ndugu zenu tu mwapata nini zaidi ya wengine? Je!, Watu wa mataifa hawafanyi vivyo hivyo? \v 48 Kwa hiyo yawapasa kuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

1
06/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Zingatia kutotenda matendo ya haki mbele ya watu ili kujionyesha, vinginevyo hutapata thawabu kutoka kwa Baba aliye mbinguni. \v 2 Hivyo basi unapotoa usipige tarumbeta na kujisifu mwenyewe kama wanafiki wanavyofanya katika masinagogi na katika mitaa, ili kwamba watu wawasifu. Kweli nawaambia, wamekwisha kupokea thawabu yao.

1
06/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Lakini wewe unapotoa, mkono wako wa kushoto usijue kinachofanywa na mkono wa kulia, \v 4 ili kwamba zawadi yako itolewe kwa siri. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako.

1
06/05.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 5 Na unapokuwa ukiomba, usiwe kama wanafiki, kwa kuwa wanapenda kusimama na kuomba kwenye masinagogi na kwenye kona za mitaani, ili kwamba watu wawatazame. Kweli nawaambia, wamekwishapokea thawabu yao. \v 6 Lakini wewe, unapo omba, ingia chumbani. Funga mlango, na uombe kwa kwa Baba yako aliye sirini. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako. \v 7 Na unapokuwa ukiomba, usirudie rudie maneno yasiyo na maana kama mataifa wanavyofanya, kwa kuwa wanafikiri kwamba watasikiwa kwa sababu ya maneno mengi wanayosema.

1
06/08.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 8 Kwa hiyo, usiwe kama wao, kwa kuwa Baba yako anatambua mahitaji yako hata kabla hujaomba kwake. \v 9 Hivyo basi omba hivi: Baba yetu uliye mbinguni, ulitukuze jina lako. \v 10 Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni.

1
06/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Utupatiye leo mkate wetu wa kila siku. \v 12 utusamehe deni zetu, kama nasi tunavyowasamehe wadeni wetu. \v 13 Na usitulete katika majaribu, lakini utuepushe kutoka kwa yule mwovu.'

1
06/14.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 14 Ikiwa mtawasemehe watu makosa yao, Baba yako aliye mbinguni pia atawasamehe ninyi. \v 15 Lakini ikiwa hamtawasamehe makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.

1
06/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Zaidi ya yote, unapokuwa umefunga, usioneshe sura ya huzuni kama wanafiki wanavyofanya, kwa kuwa wanakunja sura zao ili kwamba watu wawatambue wamefunga. Kweli ninakuambia, wamekwisha kupokea thawabu yao. \v 17 Lakini wewe, unapokuwa umefunga, paka mafuta kichwa chako na uoshe uso wako. \v 18 Hivyo haitakuonesha mbele ya watu kuwa umefunga, lakini tu itakuwa kwa Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini, atakupa thawabu yako.

1
06/19.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 19 Usijitunzie hazina yako mwenyewe hapa duniani, ambapo nondo na kutu huharibu, ambapo wezi huvunja na kuiba. \v 20 Badala yake, jitunzie hazina yako mwenyewe mbinguni, ambapo wala nondo wala kutu hawezi kuharibu, na ambapo wezi hawawezi kuvunja na kuiba. \v 21 Kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo na moyo wako utakapokuwepo pia.

1
06/22.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 22 Jicho ni taa ya mwili. Kwa hiyo, ikiwa jicho lako ni zima, mwili wote utajazwa na nuru. \v 23 Lakini ikiwa jicho lako ni bovu, mwili wako wote umejaa giza totoro. Kwahiyo, ikiwa nuru ambayo imo ndani yako ni giza hasa, ni giza kubwa kiasi gani! \v 24 Hakuna hata mmoja anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa kuwa atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au la sivyo atajitoa kwa mmoja na kumdharau mwingine. Hamuwezi kumtumikia Mungu na mali.

1
06/25.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 25 Kwa hiyo nakuambia, usiwe na mashaka kuhusu maisha yako, kuwa utakula nini au utakunywa nini, au kuhusu mwili wako, utavaa nini. Je! Maisha si zaidi ya chakula na mwili zaidi ya mavazi? \v 26 Tazama ndege walioko angani. Hawapandi na hawavuni na hawakusanyi na kutunza ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha wao. Je ninyi si wa thamani zaidi kuliko wao?

1
06/27.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 27 Na ni nani miongoni mwenu kwa kujihangaisha anaweza kuongeza dhiraa moja kwenye uhai wa maisha yake? \v 28 Na kwa nini mna kuwa na wasiwasi kuhusu mavazi? Fikiria kuhusu maua kwenye mashamba, jinsi yanavyokua. Hayafanyi kazi na hayawezi kujivisha. \v 29 Bado ninawaambia, hata Sulemani katika utukufu wake wote hakuvikwa kama mojawapo ya haya.

1
06/30.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 30 Ikiwa Mungu anayavalisha majani katika mashamba, ambayo yadumu siku moja na kesho yanatupwa katika moto, je ni kwa kiasi gani atawavalisha ninyi, ninyi wenye imani ndogo? \v 31 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi nakusema, 'Je tutakula nini?' au "Je tutakunywa nini?" au "Je tutavaa nguo gani?"

1
06/32.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 32 Kwa kuwa mataifa wanatafuta mambo haya, na Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnahitaji hayo. \v 33 Lakini kwanza tafuteni ufalme wake na haki yake na haya yote yatakabidhiwa kwako. \v 34 Kwa hiyo, usione shaka kwa ajili ya kesho, kwa kuwa kesho itajishughulikia yenyewe. Kila siku inatosha kuwa na tatizo lake yenyewe.

1
07/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Usihukumu, nawe usije ukahukumiwa. \v 2 Kwa hukumu unayohukumu, nawe utahukumiwa. Na kwa kipimo unachopima na wewe pia utapimiwa hicho hicho.

1
07/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Na kwa nini unatazama kipande cha mti kilichoko kwenye jicho la ndugu yako, lakini hutambuwi kipande cha gogo ambalo limo katika jicho lako? \v 4 Unawezaje kusema kwa ndugu yako, ngoja nikutolee kipande kilichomo kwenye jicho lako, wakati kipande cha gogo kimo ndani ya jicho lako? \v 5 Mnafiki wewe; kwanza toa gogo lililomo kwenye jicho lako, na ndipo utakapoweza kuona vizuri na kukitoa kipande cha mti kilichomo kwenye jicho la ndugu yako.

1
07/06.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 6 Usiwape mbwa kilicho kitakatifu, na usiwarushie nguruwe lulu mbele yao. Vinginevyo wataviharibu na kuvikanyaga kwa miguu, na tena watakugeukia wewe na kukurarua vipande vipande.

1
07/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Omba, nawe utapewa. Tafuta, nawe utapata. Bisha hodi, na wewe utafunguliwa. \v 8 Kwa yeyote anayeomba, hupokea. Na kwa yeyote anayetafuta, hupata. Na kwa mtu ambaye anayebisha hodi, atafunguliwa. \v 9 Au kuna mtu miongoni mwenu ambaye, ikiwa mtoto wake amemwomba kipande cha mkate atampa jiwe? \v 10 Au ikiwa atamwomba samaki, na yeye atampa nyoka?

1
07/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Kwa hiyo, ikiwa ninyi mlio waovu mnajua kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, Je! Ni kiasi gani zaidi Baba aliye mbinguni atawapa vitu vizuri wale wanao muomba yeye? \v 12 Kwa sababu hiyo, unapotaka kufanyiwa kitu chochote na watu wengine, nawe pia itakupasa kuwafanyia hivyo hivyo wao. Kwa kuwa hiyo ni sheria na manabii.

1
07/13.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 13 Ingieni kwa kupitia geti jembamba. Kwa kuwa geti ni pana na njia ni pana inayoongoza kwenye uharibifu, na kuna watu wengi wanaopitia njia hiyo. \v 14 Geti ni jembamba, Geti jembamba ni njia inayongooza katika uzima na ni wachache wanaoweza kuiona.

1
07/15.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 15 Jihadhari na manabii wa uongo, wanaokuja wamevaa ngozi ya kondoo, lakini kweli ni mbweha wakali. \v 16 Kwa matunda yao mtawatambua. Je watu wanaweza kuvuna matunda kwenye miba, au mtini kwenye mbengu ya mbaruti? \v 17 Kwa jinsi hiyo, kila mti mzuri huzaa matunda mazuri, lakini mti mbaya huzaa matunda mabaya.

1
07/18.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 18 Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. \v 19 Kila mti ambao hauzai matunda mazuri utakatwa na kutupwa katika moto. \v 20 Hivyo basi, utawatambua kutokana na matunda yao.

1
07/21.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 21 Si kila mtu aniambiaye mimi, 'Bwana, Bwana,' ataingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni yule pekee atendaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. \v 22 Watu wengi wataniambia siku hiyo, 'Bwana, Bwana, hatukutoa unabii kwa jina lako, hatukutoa mapepo kwa jina lako, na kwa jina lako tulifanya matendo mengi makuu?' \v 23 Ndipo nitawaambia wazi, 'sikuwatambua ninyi! Ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu!'

1
07/24.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 24 Kwa hiyo, kila mmoja asikiaye maneno yangu na kutii atafanana na mtu mwenye hekima aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba. \v 25 Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuweza kuanguka chini, kwa kuwa ilikuwa imejengwa juu ya mwamba.

1
07/26.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 26 Lakini kila mtu anayesikia neno langu na asilitii, atafananishwa na mtu mpumbavu aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga. \v 27 Mvua ikaja, mafuriko yakaja, na upepo ukaja na kuipiga nyumba hiyo. Na ikaanguka, na uharibifu wake ukakamilika."

1
07/28.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 28 Ulifika wakati ambao Yesu alipomaliza kuongea maneno haya, makutano walishangazwa na mafundisho yake, \v 29 kwa kuwa alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama waandishi wao.

1
08/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Wakati Yesu aliposhuka chini kutoka mlimani, umati mkubwa ulimfuata. \v 2 Tazama, mkoma alikuja na kusujudu mbele yake, akasema, "Bwana, ikiwa uko tayari, unaweza kunifanya niwe safi". \v 3 Yesu akanyoosha mkono wake na kumgusa, akasema, "Niko tayari. Uwe msafi." Hapo hapo alitakaswa ukoma wake.

1
08/04.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 4 Yesu akamwambia, "Angalia kwamba usiseme kwa mtu yeyote. Shika njia yako, na jioneshe mwenyewe kwa kuhani na utoe zawadi ambayo Musa aliagiza, kwa ajili ya ushuhuda kwao"

1
08/05.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 5 Wakati Yesu alipofika Kapernaumu, Jemedari akaja kwake akamuuliza \v 6 akisema, "Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani amepooza na ana maumivu ya kutisha." \v 7 Yesu akamwambia, "Nitakuja na kumponya".

1
08/08.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 8 Jemedari akajibu na kumwambia, "Bwana, mimi si wathamani hata uje na kuingia ndani ya dari yangu, sema neno tu na mtumishi wangu ataponywa. \v 9 Kwa kuwa mimi pia ni mtu niliye na mamlaka, na ninao askari walio chini yangu. Nikisema kwa huyu "Nenda' na huenda, na kwa mwingine 'Njoo' na yeye huja, na kwa mtumishi wangu, 'Fanya hivi,' na yeye anafanya hivyo" \v 10 Wakati Yesu aliposikia haya, alishangazwa na kuwaambia wale waliokuwa wakimfuata, "Kweli ninawaambia, Sijapata kuona mtu mwenye imani kama huyu katika Israel.

1
08/11.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 11 Ninawambieni, wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, wataketi katika meza pamoja na Abrahimu, Isaka, na Yakobo, katika ufame wa mbinguni. \v 12 Lakini watoto wa ufalme watatupwa katika giza la nje, ambapo kutakuwa na kilio na kusaga meno." \v 13 Yesu akamwambia Jemadari, "Nenda! Kama ulivyokwisha amini, na itendeke hivyo kwako". Na mtumishi aliponywa katika saa hiyo.

1
08/14.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 14 Wakati Yesu alipofika kwenye nyumba ya Petro, alimwona mama mkwe wake na Petro amelala akiwa mgonjwa wa homa. \v 15 Yesu akamgusa mkono wake, na homa yake ikamwacha. kisha akaamka akaanza kumhudumia.

1
08/16.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 16 Na ilipofika jioni, watu wakamletea Yesu wengi waliotawaliwa na pepo. Akawafukuza pepo na wale walio wagonjwa akawaponya. \v 17 Kwa jinsi hii yalitimia yale yaliyo kwisha kunenwa na Isaya nabii, "Yeye mwenyewe alichukua magonjwa yetu na alibeba maradhi yetu"

1
08/18.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 18 Kisha Yesu alipoliona kusanyiko limemzunguka, alitoa maelekezo ya kwenda upande mwingine wa Bahari ya Galilaya. \v 19 Kisha mwandishi akaja kwake na kumwambia, "Mwalimu, nitakufuata popote utakapoenda." \v 20 Yesu akamwambia, "Mbweha wana mashimo, na ndege wa angani wana viota, lakini mwana wa Adamu hana sehemu ya kulaza kichwa chake."

1
08/21.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 21 Mwanafunzi mwingine akamwambia, "Bwana, niruhusu kwanza niende kumzika baba yangu." \v 22 Lakini Yesu akamwambia, "Nifuate, na uwaache wafu wazike wafu wao."

1
08/23.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 23 Yesu alipoingia kwenye mtumbwi, wanafunzi wake wakamfuata mtumbwini. \v 24 Tazama, ikainuka dhoruba kuu juu ya bahari, kiasi kwamba mtumbwi ulifunikwa na mawimbi. Lakini Yesu alikuwa amelala. \v 25 Wanafunzi wakaja kwake na kumwamsha wakisema, "Bwana, tuokoe sisi, tunaelekea kufa!"

1
08/26.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 26 Yesu akawaambia, "kwa nini mnaogopa, ninyi wenye imani ndogo?" Ndipo akaamka na kuukemea upepo na bahari. Kisha kukawa na utulivu mkuu, \v 27 wanaume wakashikwa na mshangao wakasema, "Huyu mtu niwa namna gani, kwamba hata pepo na bahari vinamtii yeye?"

1
08/28.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 28 Wakati Yesu alipokuwa amekuja upande mwingine wa nchi ya Magadala, wanaume wawili waliotawaliwa na pepo walikutana naye. Walikuwa wakitokea makaburini na walikuwa wakifanya vurugu sana, kiasi kwamba hakuna msafiri angeweza kupita njia ile. \v 29 Tazama, walipaza sauti na kusema, "Tuna nini cha kufanya kwako, mwana wa Mungu? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati kufika?"

1
08/30.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 30 Sasa kundi kubwa la nguruwe lilikuwa likichunga, hapakuwa mbali sana walipokuwa, \v 31 pepo waliendelea kulalamika kwa Yesu na kusema. "Ikiwa utatuamuru kutoka, tupeleke kwenye kundi la nguruwe." \v 32 Yesu akawaambia, "Nendeni!" Pepo wakawatoka na kwenda kwa nguruwe. Na tazama, kundi lote likashuka kutoka mlimani kuteremkia baharini na lote likafia majini.

1
08/33.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 33 Wanaume waliokuwa wakichunga nguruwe walikimbia. Na walipoenda mjini wakaelezea kila kitu, hususani kilichotokea kwa wanaume waliotawaliwa na mapepo. \v 34 Tazama, mji mzima ukaja kukutana na Yesu. Walipomwona, walimsihi aondoke kwenye mkoa wao.

1
09/01.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 1 Yesu akaingia kwenye boti, akavuka na akafika kwenye mji alipokuwa anaishi. \v 2 Tazama, wakamletea mtu aliyepooza amelazwa kwenye godoro. alipooiona imani yao, Yesu akamwambia mtu aliyepooza, "Mwanangu, uwe na furaha, Dhambi zako zimesamehewa"

1
09/03.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 3 Tazama, Baadhi ya walimu wa sheria wakasemezana wao kwa wao, "Huyu mtu anakufuru" \v 4 Yesu akatambua mawazo yao na kusema, "Kwa nini mnawaza maovu moyoni mwenu? \v 5 Kipi kilicho rahisi kusema, 'Dhambi zako zimesamehewa' au kusema, 'Simama na utembee?' \v 6 Lakini mtambue ya kwamba Mwana wa Adamu anao uwezo wa kusamehe dhambi..." aliyasema haya kwa yule aliyepooza, "Simama, chukua godoro lako, na uende nyumbani kwako"

1
09/07.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 7 Ndipo yule mtu akasimama na kuondoka kwenda nyumbani kwake. \v 8 Makutano walipoona hayo, walishangaa na kumsifu Mungu, ambaye amewapa uwezo huo watu. \v 9 Na Yesu alipokuwa akipita kutoka hapo, alimwona mtu ambaye aliitwa kwa jina la Mathayo, ambaye alikuwa amekaa sehemu ya watoza ushuru. Naye akamwambia, "Nifuate mimi" Naye akasimama na kumfuata.

1
09/10.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 10 Na Yesu alipoketi ili ale chakula ndani ya nyumba, wakaja watoza ushuru wengi na watu waovu wakashiriki chakula pamoja na Yesu na wanafunzi wake. \v 11 Ndipo Mafarisayo walipoona hayo, wakawaambia wanafunzi "Kwa nini mwalimu wenu anakula chakula pamoja na watoza ushuru na watu waovu?"

1
09/12.txt Normal file
View File

@ -0,0 +1 @@
\v 12 Yesu aliposikia hayo, naye alisema " Watu walio na afya nzuri hawahitaji mganga, isipokuwa wale walio wagonjwa. \v 13 Inawapasa muende mkajifunze maana yake, "Ninapenda rehema na siyo dhabihu" Kwa kuwa nilikuja, si kwa wenye haki kutubu, lakini kwa wenye dhambi.

Some files were not shown because too many files have changed in this diff Show More