sw_mat_text_reg/02/13.txt

1 line
450 B
Plaintext

\v 13 Baada ya kuwa wameondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto na kusema, "Inuka, mchukue mtoto na mama yake na mkimbilie Misri. Bakini huko mpaka nitakapowaambia, kwa kuwa Herode atamtafuta mtoto ili amwangamize. \v 14 Usiku huo Yusufu aliamka na kumchukua mtoto na mama yake na kukimbilia Misri. \v 15 Aliishi huko hadi Herode alipo kufa. Hii ilitimiza kile Bwana alichokuwa amenena kupitia nabii, "Kutoka Misri nimemwita mwanangu."