forked from WA-Catalog/sw_tn
935 B
935 B
Agizo la neno la Bwana kwa Israel kwa Mkono wa Malaki.
"Bwana alizungumza haya maneno kwa waisrael kupitia Malaki"
Kwa mkono wa Malaki
kupitia kutenda kwa Malaki
Lakini wasema, "Umetupenda kwa namna gani?"
Hili swali linaonyesha shaka, au maswali juu ya ukweli wa neno la Mungu. Mungu anatumia swali kuwakemea watu. Tafsiri mbadala: lakini wasema, "Hujatupenda!"
Hakuwa Esau ndugu yake Yakobo?
"Nitawaambia jinsi ninavyowapenda ninyi. mnajua kwamba Esau ni ndugu yake Yakobo."
Asema Bwana
Bwana mwenye kweli amesema haya"
Nimempenda Yakobo
Bwana alichagua kuwa na mahusiano na Yakobo na kuwa Mungu ya Yakobo.
Nimemchukia Esau
Bwana alimkataa Esau
Nimeifanya Milima yake kuwa ya uharibifu na kuteketezwa
"Nimeifanya milima yake kuwa haifai kukaa ndani yake"
Na nimeufanya urithi wake kuwa sehemu ya mbweha wa mwituni
"Na nimeifanya nchi anayorithi kuwa jangwa ambapo wanyama pekee wanaweza kuishi"