sw_tn_fork/1ti/05/09.md

45 lines
1.6 KiB
Markdown

# aandikishwe kama mjane
inaonekana kulikuwapo na orodha, iliyoandikwa au la, ya wajane. washiriki wa kanisa waliyatimiza mahitaji hayo ya wanawake ya makazi, mavazi, na chakula; na wanawake hawa walitarajiwa kujitolea maisha yao kwa kuwahudumia jumuiya ya kikristo.
# aliye juu ya umri wa miaka sitini
Wajane ambao walikuwa wadogo chini ya miaka sitini wanaweza kuolewa tena, na hivyo Kanisa linapaswa kuwatunza tu wajane ambao walikuwa na umri zaidi ya sitini.
# mke wa mume mmoja
Maana inawezekana ni 1) yeye alikuwa daima mwaminifu kwa mumewe au 2) na hajapewa talaka na mume wake na kuolewa na mtu mwingine.
# Awe najulikana kwa matendo mema
Hii inaweza andikwa kama "Watu lazima waweze kushuhudia kwa matendo yake mema"
# ameniosha miguu
"kufanya kazi kusaidia." Kuosha miguu michafu ya watu ambao wamekuwa wakitembea katika uchafu na matope ni picha ya kukutana na mahitaji ya watu wengine na kufanya maisha yawe yafuraha kwao.
# Waaminio
Baadhi ya matoleo hutafsiri "waamini" hapa kama, "Watakatifu" au "watu wa Mungu." Wazo muhimu ni kwa kutaja waumini wa Kikristo.
# amefuata kazi zote njema
"ni maalumu kwa ajili ya kufanya matendo mema"
# ambaye si mdogo kuliko sitini
Kama Paulo atakapo elezea kwa 5: 11-16, wajane waliokuwa na umri wa miaka midogo kuliko 60 wanaweza kuolewa tena. Kwa sababu hiyo jumuiya ya kikristo walikuwa wakuwatunza wajane ambao walikua na umri zaidi ya miaka sitini.
# amekua mkarimu kwa wageni
"amekaribisha wageni katika mji wake"
# aliwasaidia watu wenye taabu
Hapa "taabu" linaweza kutumika kama "yeye aliewasaidia wale ambao wanateseka"
# amekua akijitoa kwa kila kazi njema
"amejitoa kwa kufanya kila aina ya matendo mema"