forked from WA-Catalog/sw_tn
37 lines
1.3 KiB
Markdown
37 lines
1.3 KiB
Markdown
# Vivyo hivyo.
|
|
|
|
Neno hili huashiria mlingano wa ulimi kwa rijamu za farasi na usukani wa meli katika mistari iliyotangulia.
|
|
|
|
# Hujisifia mambo makuu sana
|
|
|
|
"mambo" ni ujumla wa vitu vyote ambavyo watu hawa wanajisifia.
|
|
|
|
# Angalia
|
|
|
|
"fikiri kuhusu"
|
|
|
|
# Jinsi msitu ulivyo mkubwa unawashwa na cheche moja!
|
|
|
|
"Ulimi mdogo wa moto unaweza kuwasha moto utakao unguza miti mingi!"
|
|
|
|
# Ulimi pia ni moto.
|
|
|
|
Kama moto unavyo uunguza na kuteketeza vyote vinavyochomwa, ulimi, husimama badala ya mambo ambayo mtu huyatamka, yanaweza kuwaumiza watu vibaya. "Ulimi ni kama moto."
|
|
|
|
# Ulimwengu wa uovu umewekwa katikati mwa viungo vya mwili wetu.
|
|
|
|
"Ni sehemu ndogo ya mwili wetu, lakini una uwezo wa kufanya dhambi katika aina zote za mambo."
|
|
|
|
# Ambao hunajisi mwili wote.
|
|
|
|
Hii inaweza kutafsiriwa kama sentensi mpya. "Inaweza kutufanya sisi tusimpendeze Mungu kabisa" au "Inaweza ikatufanya sisi tusikubalike kwa Mungu."
|
|
|
|
# Na huweka katika moto njia ya uzima.
|
|
|
|
Msemo huu "njia ya uzima" una maana ya maisha yote ya mtu. "na unaweza kuharibu maisha yote ya mtu."
|
|
|
|
# Na wenyewe unachomwa katika moto katika jehanamu.
|
|
|
|
Neno "wenyewe" limesimama badala ya ulimi. Pia, hapa neno "jehanamu" limesimama badala ya nguvu za uovu au nguvu za shetani. Hii ingeweza kutafsiriwa kama kishazi kazi: "kwa sababu shetani huutumia kwaajili ya uovu."
|
|
|