sw_tn_fork/gal/05/01.md

778 B

Sentensi Unganishi

Paulo anatumia mfano kwa kuwakumbusha waumini kutumia uhuru wao katika Kristo kwa sababu sheria yote imekamilika katika kumpenda jirani kama sisi wenyewe.

Ni kwa Uhuru

Tafsiri inahitaji kusisitiza "uhuru" kinyume cha utumwa uliozungumzwa katika mistari iliyotangulia

Ni kwa uhuru ambao Kristo ametuweka sisi huru

"ili kwamba tuweze kuwa kuwa huru maana Kristo ametuweka huru"

simameni imara

kusimama imara hapa inawakilisha hali ya kutobadilika. Hali ya kutobadilika inaweza kuelezwa kwa uwazi. "msikubali hoja za watu wengine wanaowafundisha vitu tofauti" au " dhamirieni kuwa huru"

kama mtakuwa mmetahiriwa

Paulo anatumia neno 'tohara' kama lugha ya mfano au picha kumaanisha dini ya kiyahudi. "Kama mtarudi kwenye Dini ya Kiyahudi"