1.3 KiB
Katika mwaka wa thelathini na nane wa Azaria mfalme wa yuda
mwaka wa nane wa Azaria mfalme wa Yuda** - Inaweza kuelezwa wazi kwamba hii ni miaka thelathini na nane mwaka wa utawala wake. "Katika mwaka wa 38 wa utawala wa Azaria mfalme wa Yuda"
Zakaria mwana wa Yeroboamu
Huyu Yeroboamu alikuwa mfalme wa pili wa Israeli ambaye alikuwa na hilo jina. Alikuwa mwana wa mfalme Yoashi.
alitawala juu ya Israeli katika Samaria kwa miezi sita
Samaria ni mji ambao Zekaria aliishi huko alipokuwa mfalme wa Israeli. "aliishi Samaria na kutawala juu ya Israeli kwa miezi sita"
Alifanya yaliyo maovu
"Zekaria alifanya yaliyo maovu"
yaliyo maovu katika uso wa Yahwe
Uso wa Yahwe unawakilisha hukumu ya Yahwe. "yaliyo maovu katika hukumu ya Yahwe" au "kile Yahwe afikiriacho kuwa uovu"
Hakuziacha dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti
Kuziacha`dhambi inawakilisha kuzifanya hizo dhambi. "Zekaria hakukataa kufanya dhambi za Yeroboamu mwana wa Nabeti" au "aliasi kama Yeroboamu mwana wa Nabeti alivyo asi"
Yeroboamu mwana wa Nabeti
Huyu Yeroboamu alikuwa mfalme wa kwanza kati ya makabila kumi ya kaskazini ambayo yaliutengeneza ufalme wa Israeli.
ambaye aliisababisha Israeli kuasi
Hapa neno "Israeli" linawakilisha watu wa ufalme wa Israeli. "ambao walisababisha watu wa Israeli kuasi"