sw_tn_fork/1ki/03/15.md

1.6 KiB

ndoto

Ndoto ni kitu ambacho huwapata watu katika akili zao wanapokuwa katika usingizi. Hutokea na watu wakaona kama ni katu halisi na kumbe sivyo. Wakati mwingine Mungu hutumia ndoto kufikisha ujumbe kwa watu wake.

Yerusalemu

Kwa asili Yerusalmu ulikuwa mji wa Wakanaani ambao b aadaye ulikuja kuwa mji wa muhimu wa Israeli. Mjihuu uko kilomita 34 magharibi mwa bahari ya chumvi na kaskazini kidogo mwa Bethelehemu. Mpaka sasa bado ni mji mkuu wa Israeli.

sanduku la agano la Bwana, sanduku laamri ya agano, sanduku la BWANA

sentensi hizi zinamaanisha sanduku maalumu ambalo limesakafiwa kwa dhahabu, ambalo ndani mwake kulikuwa na vile vidonge viwili vya mawe vilivyokuwa vimeandikwa amri kumi za Mungu. Pia lilikuwa na fimbo ya Haruni pamoja na jagi la mana.

Bwana

Neno "Bwana" linamaanisha mtu aliye naumiliki fulani pia mwenye mamlaka juu ya watu. Lina hili linapoanza kwa herufi kubwa humaanisha Mungu.

sadaka za kuteketezwa, sadaka za moto

sadaka za kuteketezwa zilikuwa ni aina za sadaka ambazo zilikuwa zimechomwa kwa moto madhabahuni. Zilitengenezwa kwa ajili ya fidia ya dhambi za watu. Sadaka hizi zilijulikana pia kama "sadakaza moto."

sadaka za amani

"sadaka za amani" zilikuwa ni moja kati ya sadaka nyingi ambazo Mungu aliwaamuru Waisraeli kutoa. Pia ziliitwa "sadaka za shukurani" au "sadaka za amani"

sherehe

Neno "sherehe" linamaanisha tukio ambalo makundi ya watu walikula chakula kingi kwa pamoja kwa lengo la kufurahia jambo fulani. Wakati mwingine kunakuwa na chakula maalumu.

mtumishi, mtumwa, utumwa

Neno "mtumishi" linaweza kumaanisha "mtumwa" lenye maana ya mtu anayetumika kwa mtu mwingine kwa kupenda yeye au kwa kulazimishwa.