sw_tn_fork/1co/15/35.md

1.2 KiB

Sentensi unganishi

Paulo anatoa maelezo mahususi juu ya ufufuo wa miili ya waumini utakavyotokea. Anaeleza juu ya miili ya asili na miili ya kiroho kwa kulinganisha Adamu wa kwanza na Aadamu wa mwisho ambaye ni Kristo.

Lakini mtu mwingine atasema, "Jinsi gani wafu wanafufuliwa? Nao watakuja na aina gani ya mwili?"

Hapa inaweza kumaanisha 1)mtu alikuwa akijiho kwa nia njema au) 2) mtu anauliza swali ili kukejeli swala la ufufuo. kwa maneno mengine ni kusema "Baadhi ya watu watasema kwamba hawapati picha jinsi Mungu atakavyo wafufua wafu, na aina gani ya mwili Mungu atawapa katika ufufuo."

mtu mwingine atasema

"mtu atauliza"

Nao watakuja na aina gani ya mwili

hii ni sawa na kuuliza kwamba, je utakuwa mwili halisi au mwili wa kiroho? je mwili huo utakuwa na umbo gani? je mwili huo utatengenezwa kwa vitu gani?

Wewe ni mjinga sana! Kile ulichopanda

Paulo anaonekana kama vile anazungumza na mtu mmoja "Wewe" ni neno kuonyesha umoja.

Wewe ni mjinga

" hujui kabisa kuhusu mambo haya yote"

Kile ulichopanda hakiwezi kuanza kukua isipokuwa kimekufa.

Kama vile mbegu isivyo weza kuota mpaka ifukiwe ardhini. Vile vile mtu lazima afe kwanza kabla ya kufufuliwa na Mungu