1.2 KiB
1 Wakorintho 04 Maelezo ya Jumla
Dhana maalum katika sura hii
Kiburi
Paulo analinganisha Wakorintho walio na kiburi na mitume walio wanyenyekevu. Waumini wa Korintho hawakuwa na sababu ya kuwa na kiburi. Yote waliyokuwa nayo, na waliyokuwa; yalikuwa zawadi kutoka kwa Mungu. (See: rc://en/tw/dict/bible/kt/apostle)
Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii
Mifano
Paulo anatumia mifano nyingi katika sura hii. Anaelezea mitume kama watumishi. Paulo anazungumza juu ya gwaride la ushindi ambapo mitume watakuwa ni wafungwa ambao watauawa. Anatumia fimbo ili kumaanisha adhabu. Anajiita baba yao kwa sababu yeye ni "baba yao wa kiroho." (See: rc://en/ta/man/translate/figs-metaphor]] and [[rc://en/tw/dict/bible/kt/spirit)
Kinaya
Paulo anatumia kinaya kuwaaibisha Wakorintho kwa kuwa na kiburi. Waumini wa Korintho wanatawala lakini mitume wanateseka. (See: rc://en/ta/man/translate/figs-irony)
Maswali ya uhuishaji
Paulo anatumia maswali kadhaa ya uhuishaji katika sura hii. Anayatumia kusisitiza neno muhimu anapofundisha Wakorintho. (See: rc://en/ta/man/translate/figs-rquestion)