sw_tn_fork/isa/62/03.md

21 lines
707 B
Markdown

# Pia utakuwa taji la uzuri mikononi mwa Yahwe, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako
Hizi zina maana moja na zinaunganishwa kwa ajili ya msisitizo. Zinasema ya kwamba Yerusalemu utakuwa mji wa kifalme chini ya nguvu na mamlaka ("mkono") ya Mungu.
# haitakuwa kwako tena ... kusemwa, "Ukiwa"
Hizi zina maana moja na zinaunganishwa kwa ajili ya msisitizo.
# haitasemwa kwako tena
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "Watu hawatasema tena juu yako"
# wala nchi yako haitasemwa tena
Hii inaweza kuelezwa katika hali ya kutenda. "wala watu hawatasema tena juu ya nchi yako"
# na nchi yako itaolewa
Hii ina maana Yahwe atawapenda watu wa Israeli na atakuwa nao daima kama alivyo mume.