1.2 KiB
Kwa maana kile ambacho sheria ilishindwa kufanya kwa sababu ilikuwa dhaifu katika mwili, Mungu alifanya
Hapa sheria inaelezwa kama mtu ambayo hakuweza kuvunja nguvu ya dhambi. "Maana sheria haikuwa na nguvu ya kutuzuia sisi kutenda dhambi, kwasababu dhambi iliyokuwa ndani yetu ilikuwa na nguvu sana. Lakini Mungu aliweza kutuzuia sisi kutenda dhambi."
katika mwili
"Kwasababu ya asili ya dhambi ya watu"
Yeye...alimtuma Mwana wake pekee kwa mfano wa mwili wa dhambi...sadaka ya dhambi...aliihukumu dhambi
Mwana wa Mungu aliiridhisha hasira takatifu ya Mungu dhidi ya dhambi kwa kuutoa mwili wake na uhai wa kibinadamu kama sadaka ya kudumu ya dhambi.
Mwana
Hili ni jina la muhimu kwa Yesu, Mwana wa Mungu.
kwa mfano wa mwili wa dhambi
"aliyeonekana kama mwanadamu mwenye dhambi mwingine yeyote"
kuwa sadaka ya dhambi
"ili kwamba afe kama sadaka kwajili ya dhambi zetu"
na alihukumu dhambi katika mwili
"na Mungu alivunja nguvu ya dhambi kupitia mwili wa Mwana wake"
mahitaji ya sheria yaweze kutimizwa kwetu
"tuweze kutimiza mahitaji ya sheria"
sisi ambao tusioenenda kwa jinsi ya mwili
"sisi ambao hatuzitii tamaa zetu za dhambi"
bali kulingana na yule Roho
"lakini wale ambao wanamtii Roho Mtakatifu"