sw_tn/rom/02/05.md

1.2 KiB

Sentensi unganishi:

Paulo anaendelea kuwakumbusha watu kwamba watu wote ni waovu.

Lakini ni kwa kadri ya ugumu wako na moyo wako usiotubu

Paulo anamfananisha mtu aliyekataa kusikia na kumtii Mungu na kitu kigumu, kama jiwe. Moyo unamaanisha mtu mzima. "Ni kwa sababu umekataa kusikiliza na kutubu"

Ugumu na moyo usiotubu

Mstari "moyo usiotubu" inaelezea neno "ugumu"

Unajiwekea mwenyewe akiba ya ghadhabu

Neno "kujiwekea" inamaanisha mtu aliyekusanya mali zake na kuziweka sehemu salama. Paulo anasema badala ya mali mtu anakusanya adhabu ya Mungu. Kadri unavyoendelea bila kutubu, ndivyo adhabu inavyozidi kuwa kubwa. "unaifanya adhabu yako inakuwa mbaya zaidi"

siku ya ghadhabu... siku ambayo Mungu atadhihirisha hukumu yake ya haki

Hii inamaanisha siku hiyo hiyo. "Ambayo Mungu atawaonyesha watu kuwa ana hasira na anahukumu watu wote kwa haki."

Kulipa

"Kutoa tuzo ya haki au adhabu"

kwa kila mtu kipimo sawa kwa matendo yake

"kutokana na kila mtu alivyofanya"

Wametafuta

Hii inamaanisha kwamba walienenda kwa njia ambazo ziliwapa matokeo hasi toka kwa Mungu siku ya hukumu.

Sifa, heshima na kutokuharibika.

Walitaka Mungu awasifu na kuwaheshimu, na walitaka wasife kabisa.

Kutoharibika

Hii inamaanisha, kimwili, sio ya maadili, kuoza.