1.1 KiB
aliyeziingia mbingu
"aliyeingia mahali alipo Mungu"
Mwana wa Mungu
Hiki ni cheo muhimu kwa Yesu.
tushikilie sana imani zetu
imani na tumaini vinaongelewa kana kwamba ni vitu ambavyo mtu angeweza kuvikumbatia.
hatuna kuhani mkuu ambaye hawezi kutuhurumia... Badala, tunaye
Maneno haya yakukanusha yanalenga kuonyesha kwamba Yesu ni mwenye huruma kwa watu . AT: " tunaye kuhani mkuu anayeweza kutuhurumia...Kweli tunaye"
kiti cha enzi cha neema
"kiti cha enzi cha Mungu, pale palipo na neema" au "pale Mungu, ambaye ni neema, ameketi katika kiti chake cha enzi"
yeye ambaye kwa njia zote amekuwa akijaribiwa kama sisi
Hii inaweza kusemwa katikamfumo tendaji. AT: "yeye ambaye amevumilia majaribu katika kila hali tunayoipitia" au "ambaye movu amekuwa akimjaribu katika kila njia anavyotujaribu"
hana dhambi
"hakutenda dhambi"
kiti cha enzi cha neema
"kwemye kiti cha enzi cha Mungu palipo na neema." "kiti cha enzi" hapa kina maanisha utawala wa Mungu kama mfalme.
ili kwamba tupokee rehema na kupata neema ya kutusaidia wakati wa hitaji.
"rehema" na "neema" hapa vinaongelewa kana kwamba ni vitu ambavyo vinaweza kupewa au kupatikana.