4.9 KiB
Utangulizi wa Wagalatia
Sehemu ya 1: Utangulizi wa Ujumla
Maelezo ya Kitabu cha Wagalatia
- Paulo anatangaza mamlaka yake kama mtume wa Yesu Kristo; anasema kwamba anashangazwa na mafundisho ya uongo ambayo Wakristo wa Galatia wamekubali kutoka kwa watu wengine (1:1-10).
- Paulo anasema kwamba watu wanaokolewa kwa kumtegemea Kristo pekee, si kwa kushika sheria (1:11-2: 21).
- Mungu anaweka watu kuwa haki na yeye wakati wanapomwamini Kristo tu; mfano wa Abrahamu; laana ambayo sheria huleta (na sio njia ya wokovu); utumwa na uhuru uliolinganishwa na kuonyeshwa nao Hagari na Sara (3:1-4:31).
- Watu wanapojiunga na Kristo, huwa huru kutokana na kuzingatia sheria ya Musa. Wao pia wako huru kuishi kama Roho Mtakatifu anavyowaongoza. Wao wako huru kukataa madai ya dhambi. Wao wako huru kubeba mizigo ya wenzao (5:1-6:10).
- Paulo anawaonya Wakristo wasiamini katika kutahiriwa na kufuata sheria ya Musa. Lakini, wanapaswa kumtegemea Kristo (6:11-18).
Nani aliandika Kitabu cha Wagalatia?
Paulo aliandika 1 Wakorintho. Paulo alitoka mji wa Tarso. Alikuwa alijulikana kwa jina la Sauli katika maisha yake ya awali. Kabla ya kuwa Mkristo, Paulo alikuwa Mfarisayo. Aliwatesa Wakristo. Baada ya kuwa Mkristo, alisafiri mara kadhaa katika Ufalme wa Roma akiwaambia watu kuhusu Yesu.
Haijulikani wakati gani Paulo aliandika barua hii na mahali gani alikuwa wakati wa kuandika. Wasomi wengine wanafikiri Paulo alikuwa katika mji wa Efeso na aliandika barua hii baada ya safari yake ya pili kuenda kuwaambia watu kuhusu Yesu. Wasomi wengine wanafikiri Paulo alikuwa katika mji wa Antiokia huko Siria na akaandika barua baada ya safari yake ya kwanza.
Kitabu cha Wagalatia kinahusu nini?
Paulo aliandika barua hii kwa Wakristo Wayahudi na Wayunani katika eneo la Galatia. Alitaka kuandika dhidi ya walimu wa uongo ambao walisema kwamba Wakristo wanahitaji kufuata sheria ya Musa. Paulo alitetea injili kwa kueleza kwamba mtu anaokolewa kwa kuamini Yesu Kristo. Watu wanaokolewa kama matokeo ya Mungu kuwa wema na sio matokeo ya watu wanaofanya kazi nzuri. Hakuna mtu anayeweza kumtii kikamilifu sheria. Jaribio lolote la kumpendeza Mungu kwa kuitii sheria ya Musa litasababisha Mungu kuwahukumu. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/goodnews]], [[rc:///tw/dict/bible/kt/save]], [[rc:///tw/dict/bible/kt/faith]], [[rc:///tw/dict/bible/kt/lawofmoses]] and rc://*/tw/dict/bible/kt/works)
Je, kichwa cha kitabu hiki kinapaswa kutafsiriwaje?
Watafsiri wanaweza kuchagua kuita kitabu hiki kwa kichwa chake cha jadi, "Wagalatia." Au wanaweza kuchagua kichwa cha wazi zaidi, kama "Barua ya Paulo kwa Kanisa la Galatia." (See: rc://*/ta/man/translate/translate-names)
Sehemu ya 2: Dhana muhimu za Kidini na za Kitamaduni
Ina maana gani "kuishi kama Wayahudi" (2:14)?
"Kuishi kama Wayahudi" inamaanisha kutii sheria ya Musa, ingawa mtu anategemea Kristo. Watu kati ya Wakristo wa kwanza ambao walifundisha kwamba hii ilikuwa muhimu waliitwa "Wayudaiza".
Sehemu ya 3: Masuala muhimu ya Tafsiri
Paulo alitumiaje maneno "sheria" na "neema" katika Kitabu cha Wagalatia?
Maneno haya hutumiwa kwa njia ya pekee katika Wagalatia. Kuna fundisho muhimu katika Wagalatia kuhusu maisha ya Kikristo. Chini ya sheria ya Musa, maisha ya haki au matakatifu yalihitaji mtu kuitii kanuni na masharti. Kama Wakristo, maisha matakatifu sasa yamehamasishwa na neema. Hii inamaanisha kwamba Wakristo wana uhuru katika Kristo na hawatakiwi kutii masharti ya binadamu. Lakini Wakristo wanapaswa kuishi maisha matakatifu kwa sababu wanashukuru kwamba Mungu amekuwa mwenye huruma kwao. Hii inaitwa "sheria ya Kristo." (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/righteous]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/holy]])
Paulo alimaanisha nini kwa maneno "katika Kristo," "katika Bwana," nk?
Aina hii ya kujieleza ipo katika 1:22; 2:4, 17; 3:14, 26, 28; 5:6, 10. Paulo alijaribu kueleza wazo la muungano wa karibu sana sana kati ya Kristo na waumini. Lakini, aldhamiria maana maana nyingine pia. Angalia, kwa mfano, "tunapomtafuta Mungu kutuhakikisha katika Kristo" (2:17), ambako Paulo alizungumzia kuwa mwenye haki kwa njia ya Kristo.
Tafadhali angalia utangulizi wa Kitabu cha Warumi kwa maelezo zaidi juu ya aina hii ya kujieleza.
Je, ni masuala gani muhimu katika Kitabu cha Wagalatia?
Kifungu kinachofuata ni suala la maana zaidi katika Kitabu cha Wagalatia:
- "Enyi Wagalatia msio na akili, ni nani aliyewaloga, ninyi ambao Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele ya macho yenu ya kuwa amesulibiwa? " (3:1) ULB, UDB, na matoleo mengine ya kisasa yana somo hili. Hata hivyo, matoleo ya kale ya Biblia yanaongeza, "ili msipaswe kuutii ukweli." Watafsiri wanashauriwa kutoingiza maneno haya. Hata hivyo, ikiwa katika eneo la watafsiri kuna matoleo ya kale ya Biblia ambayo yana kifungu hicho, watafsiri wanaweza kukijumuisha. Ikiwa imetafsiriwa, inapaswa kuwekwa ndani ya mabano ya mraba ([]) ili kuonyesha kwamba labda asili yao sio Wagalatia. (See: rc://*/ta/man/jit/translate-textvariants)