1019 B
Sentensi unganishi:
Paulo anawasihi walioamini wawe makini wasigeukie maneno na taratibu za wengine kwa sababu hakuna kinachoweza kuongezeka katika ukamilifu wa Mungu walio nao walioamini katika Kristo.
Ona kwamba
"Iweni makini kwamba" au "Angalieni kwamba"
kuwanasa
Paulo anazungumzia vile ambavyo mtu anavyoweza kuamini mafundisho ya uongo (kwa sababu wanaamini mafundisho ya uongo au wanapenda vitu vitu vya uongo)
falsafa
mafundisho ya kidini na imani yasiyotoka katika neno la Mungu lakini yanatokana na mawazo ya ya watu kuhusu Mungu na maisha
maneno matupu ya udanganyifu
haya ni mawazo ya upotoshaji ambayo hayatuongozi katika maisha ndani ya Kristo. Hayazalishi chochote; ni matupu au hayana thamani.
tamaduni za kibinadamu na juu ya mifumo ya dhambi ya dunia
tamaduni zote za Waisraeli na wapagani (watu wa Mataifa) mifumo ya imani haina maana.
kwa kuwa katika yeye ukamilifu wote wa Mungu unaishi kwa jinsi ya mwili
"kwa sababu asili yote ya Mungu inaishi katika mwili wa Kristo"