sw_tn/jer/16/19.md

40 lines
1.3 KiB
Markdown

# Bwana, wewe ndiwe ngome yangu
Hapa Yeremia anaanza kuzungumza na Bwana.
# ngome yangu, na kimbilio langu, na mahali pa usalama
Yeremia anazungumza juu ya Bwana kama mahali ambako adui hawezi kumshambulia. Anarudia wazo sawa mara tatu.
# mwisho wa Dunia
"kila mahali duniani"
# baba zetu walirithi udanganyifu
Hapa neno "udanganyifu" linamaanisha miungu ya uongo.
# Ubatili mtupu; hakuna faida ndani yao
Hapa maneno "Wao" na "wao" yanataja miungu ya uongo ambayo mababu waliwafundisha kuamini. Maneno mawili yanamaanisha kuwa ni sawa, na pili kuelezea jinsi 'ni tupu.'
# Watu hufanya miungu kwa ajili yao wenyewe?
Yeremia anauliza swali hili kusisitiza kwamba watu hawawezi kufanya miungu kwa ajili yao wenyewe. AT "Watu hawawezi kufanya miungu kwa ajili yao wenyewe."
# Kwa hiyo tazama!
Hapa Bwana huanza kusema. Neno "tazama" linaongeza mkazo kwa ifuatavyo. AT "Kwa hiyo, kwa kweli,"
# Nitawafanya wajue
Hapa neno "wao" linamaanisha watu kutoka mataifa. Bwana anarudia maneno haya kwa msisitizo.
# mkono wangu na nguvu zangu
Hapa neno "mkono" linamaanisha nguvu na mamlaka. Maneno mawili yanamaanisha jambo sawa na kusisitiza nguvu kubwa za Bwana. AT "nguvu yangu kubwa."
# watajua kwamba Yahweh ni jina langu
Hapa neno "jina" linahusu mtu mzima wa Yahweh. AT "watajua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wa kweli"