sw_tn/luk/08/intro.md

1.2 KiB

Luka 08 Maelezo ya Jumla

Muundo na upangiliaji

Kuna nyakati katika maelezo ya sura hii ambapo kuna mabadiliko ya ghafla katika mada. Mtafsiri hapaswi kulainisha mabadiliko haya.

Dhana maalum katika sura hii

Miujiza

Miujiza ya Yesu katika sura hii inaonyesha kwamba alikuwa na mamblaka juu ya mambo yanayozidi udhibiti wa binadamu. Inaonyesha pia kwamba kumwabudu Yesu ni jibu sahihi kwa matendo yake. (See: rc://*/tw/dict/bible/kt/authority)

Takwimu muhimu za matamshi katika sura hii

Mifano

Mfano ni hadithi fupi inayotumikiwa kwa kuonyesha fundisho ya maadili au wa kidini. Sura hii ina mfano mrefu, unaofunua ukweli kwa wale wanaomwamini Yesu. Pia yanaficha ukweli huo huo kutoka kwa wale wanaomkataa Yesu. Mifano kwa kawaida huchukua fomu ya hadithi.

Changamoto nyingine za kutafsiri katika sura hii

Kaka na Dada

Sura hii inaanzisha dhana ya kaka na dada "wa kiroho". Maandiko hutumia maneno haya kwa kutaja uhusiano kati ya Waisraeli. Hapa, wale wanaomfuata Yesu sasa wanajulikana kama kaka na dada. (See: [[rc:///tw/dict/bible/kt/spirit]] and [[rc:///tw/dict/bible/kt/brother]])

<< | >>