sw_tn/gal/05/11.md

1.5 KiB

Ndugu, kama naendelea kutangaza tohara, kwa nini bado ninateswa?

Paulo anaelezea hali ambayo haipo kwa kukazia kuwa watu wanamtesa kwasababu hahubiri watu wawe wayahudi. Hii yaweza pia kuelezwa kwa muundo tendaji. " ndugu mwaweza kuona kuwa siendelei kutangaza habari za tohara kwa sababu wayahudi wananitesa"

Ndugu

"Ndugu." Neno la kiswahili "ndugu" linamaanisha watu wa kike na wa kiume.

Kwa suala hilo kile ambacho ni kizuizi cha msalaba kitaweza kuharibiwa

Paulo anaelezea juu ya hali ambayo haipo ili kukazia kwamba watu wanamtesa kwasababu anahubiri kwamba Mungu huwasamehe watu kwasababu ya kazi ya Yesu juu ya msalaba.

jambo hilo

"kama ningekuwa bado ninasema kwamba watu wanatakiwa kuwa wayahudi"

kizuizi cha msalaba kimeondolewa

msemo huu waweza kuelezwa kwa muundo tenda: kwamba ujumbe kuhusu msalaba hauna kizuizi" au " hakuna kizuizi chochote katika mafundisho ya msalaba yanaweza kuwafanya watu wajikwae."

kizuizi cha msalaba kimeondolewa

kujikwaa inawakilisha hali ya kutenda dhambi, na kizuizi inamaanisha kitu kile kinachowafanya watu watende dhambi. katika jambo hili, dhambi ni kuukataa ukweli wa mafundisho kwamba watu wanatakiwa kuamini kuwa Yesus Kristo alikufa msalabani ili watu wawe na haki mbele za Mungu. "Mafundisho juu ya msalaba yanayowafanya watu kuukataa ukweli yamekwisha kuondolewa"

watajihasi wenyewe

Maana zinazokubalika ni 1) kukata viungo vyao vya kiume ili wawe matowashi au 2) kujikata au kujiondoa wenyewe kutoka katika ushirika wa watu wa Mungu