sw_mat_text_reg/15/36.txt

1 line
425 B
Plaintext

\v 36 Aliitwaa ile mikate saba na samaki, na baada ya kushukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi. Wanafunzi wakawapa umati. \v 37 Watu wote wakala na kutosheka. Na wakakusanya mabaki ya vipande vya chakula vilivyosalia vipande vipande, vilijaa vikapu saba. \v 38 Wote waliokula walikuwa wanaume elfu nne bila wanawake na watoto. \v 39 Kisha Yesu akauaga umati waende zao na akaingia ndani ya mashua na kwenda sehemu za Magadani.