sw_mat_text_reg/27/62.txt

1 line
482 B
Plaintext

\v 62 Siku iliyofuata ambayo ilikuwa siku baada ya maandalio, wakuu wa makuhani na Mafarisayo walikusanyika pamoja kwa Pilato. \v 63 Wakamwambia, "Bwana, tunakumbuka kuwa wakati yule mdanganyifu alipokuwa hai, alisema, 'Baada ya siku tatu atafufuka tena.' \v 64 Kwahiyo, agiza kwamba kaburi lilindwe salama mpaka siku ya tatu. Vinginevyo, wanafunzi wake wanaweza kuja kumwiba na kusema kwa watu, 'Amefufuka kutoka wafu.' Na udanganyifu wa mwisho utakuwa mbaya kuliko ule wa kwanza."