sw_mat_text_reg/27/38.txt

1 line
330 B
Plaintext

\v 38 Wanyang'anyi wawili walisulibiwa pamoja naye, mmoja upande wa kulia wake na mwingine wa kushoto. \v 39 Wale waliokuwa wakipita walimdhihaki, wakitikisa vichwa vyao \v 40 na kusema, "Wewe uliyekuwa unataka kuliharibu hekalu na kulijenga katika siku tatu, jiokoe mwenyewe! Kama ni Mwana wa Mungu, shuka chini utoke msalabani!"