sw_mat_text_reg/26/17.txt

1 line
396 B
Plaintext

\v 17 Hata siku ya kwanza ya mikate isiyotiwa chachu, wanafunzi walimwendea Yesu na kusema, "Wapi unataka tukuandalie ule chakula cha Pasaka?" \v 18 Akawaambia, "Nendeni mjini kwa mtu fulani na mwambieni, Mwalimu anasema, "Muda wangu umekaribia. Nitaitimiza Pasaka pamoja na wanafunzi wangu katika nyumba yako."" \v 19 Wanafunzi walifanya kama Yesu alivyowaagiza, na waliandaa chakula cha Pasaka.