sw_mat_text_reg/16/21.txt

1 line
487 B
Plaintext

\v 21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaambia wanafunzi kuwa ni lazima aende Yerusalemu, kuteswa kwa mambo mengi katika mikono ya wazee na wakuu wa makuhani na waandishi, kuuawa na kufufuka siku ya tatu. \v 22 Kisha Petro akamchukua Yesu pembeni na kumkemea, kwa kusema, "Jambo hili na liwe mbali nawe, Bwana, hili lisitokee kwako. \v 23 Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, "Rudi nyuma yangu shetani! Wewe ni kizuizi kwangu, kwa maana hujali mambo ya Mungu, bali mambo ya wanadamu."