sw_mat_text_reg/13/36.txt

1 line
402 B
Plaintext

\v 36 Kisha Yesu aliwaacha makutano na kwenda nyumbani. Wanafunzi wake walimwendea na kusema, "Tufafanulie mfano wa magugu ya shambani.'' \v 37 Yesu alijibu na kusema, "Apandae mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu. \v 38 Shamba ni ulimwengu; na mbegu nzuri, hawa ni wana wa ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu, na adui aliye zipanda ni ibilisi. \v 39 Na mavuno ni mwisho wa ulimwengu, na wavunaji ni malaika.