sw_mat_text_reg/06/16.txt

1 line
444 B
Plaintext

\v 16 Zaidi ya yote, unapokuwa umefunga, usioneshe sura ya huzuni kama wanafiki wanavyofanya, kwa kuwa wanakunja sura zao ili kwamba watu wawatambue wamefunga. Kweli ninakuambia, wamekwisha kupokea thawabu yao. \v 17 Lakini wewe, unapokuwa umefunga, paka mafuta kichwa chako na uoshe uso wako. \v 18 Hivyo haitakuonesha mbele ya watu kuwa umefunga, lakini tu itakuwa kwa Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini, atakupa thawabu yako.