sw_mat_text_reg/06/05.txt

1 line
529 B
Plaintext

\v 5 Na unapokuwa ukiomba, usiwe kama wanafiki, kwa kuwa wanapenda kusimama na kuomba kwenye masinagogi na kwenye kona za mitaani, ili kwamba watu wawatazame. Kweli nawaambia, wamekwishapokea thawabu yao. \v 6 Lakini wewe, unapo omba, ingia chumbani. Funga mlango, na uombe kwa kwa Baba yako aliye sirini. Ndipo Baba yako aonaye sirini atakupatia thawabu yako. \v 7 Na unapokuwa ukiomba, usirudie rudie maneno yasiyo na maana kama mataifa wanavyofanya, kwa kuwa wanafikiri kwamba watasikiwa kwa sababu ya maneno mengi wanayosema.