sw_mat_text_reg/26/39.txt

1 line
396 B
Plaintext

\v 39 Akenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, na kuomba. Akasema, "Baba yangu, kama inawezekana, kikombe hiki kiniepuke. Isiwe kama ninavyotaka mimi, bali kama utakavyo wewe." \v 40 Akawaendea wanafunzi na akawakuta wamelala usingizi, na akamwambia Petro, "Kwa nini hamkuweza kukesha nami kwa saa moja? \v 41 Kesheni na kuomba kusudi msiingie majaribuni. Roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu."