sw_mat_text_reg/27/27.txt

1 line
372 B
Plaintext

\v 27 Kisha askari wa liwali wakamchukua Yesu mpaka Praitorio na kundi kubwa la maaskari wote wakamkusanyika. \v 28 Wakamvua nguo zake na kumvika kanzu ya rangi nyekundu. \v 29 Kisha wakatengeneza taji ya miiba na kuiweka juu ya kichwa chake, na walimwekea mwanzi katika mkono wake wa kuume. Walipiga magoti mbele yake na kumkejeri, wakisema, "Salamu, Mfalme wa Wayahudi?"