sw_mat_text_reg/25/37.txt

1 line
418 B
Plaintext

\v 37 Ndipo wenye haki watamjibu na kumwambia, 'Bwana, lini tulikuona ukiwa na njaa, na kukulisha? Au una kiu na tukakupa maji? \v 38 Na lini tulikuona ukiwa mgeni, na tukakukaribisha? Au ukiwa uchi na tukakuvisha nguo? \v 39 Na lini tulikuona ukiwa mgonjwa, au katika kifungo, na tukakujia? \v 40 Na mfalme atawajibu na kuwaambia, 'Kweli nawaambia, mlichotenda hapa kwa mmoja wa ndugu zangu wadogo, mlinitendea mimi.'