sw_mat_text_reg/25/10.txt

1 line
351 B
Plaintext

\v 10 Wakati wameenda huko kununua, Bwana harusi alifika, na wote waliokuwa tayari walienda naye kwenye sherehe ya harusi, na mlango ulifungwa. \v 11 Baadaye wale wanawali wengine pia walifika na kusema, 'Bwana, bwana, tufungulie.' \v 12 Lakini alijibu na kusema, 'Kweli nawaambia, Mimi siwajui.' \v 13 Kwa hiyo angalieni, kwa kuwa hamjui siku au saa.