sw_mat_text_reg/24/06.txt

1 line
357 B
Plaintext

\v 6 Mtasikia vita na taarifa za vita. Angalieni msije mkawa na wasiwasi, kwa kuwa mambo haya hayabudi kutokea; lakini ule mwisho utakuwa bado. \v 7 Kwa kuwa taifa litainuka dhidi ya taifa jingine, na ufalme dhidi ya ufalme. Kutakuwa na njaa na matetemeko ya ardhi katika sehemu mbalimbali. \v 8 Lakini mambo haya yote ni mwanzo tu wa uchungu wa kujifungua.