sw_mat_text_reg/24/03.txt

1 line
374 B
Plaintext

\v 3 Na alipokaa katika Mlima wa Mizeituni, wanafunzi wake walimwendea kwa faragha na kusema, "Tuambie, mambo haya yatatokea lini? Kitu gani kitakuwa dalili ya kuja kwako na mwisho wa ulimwengu?" \v 4 Yesu aliwajibu na kuwaambia, "Iweni makini kwamba asije mtu akawapotosha. \v 5 Kwa kuwa wengi watakuja kwa jina langu. Watasema, 'Mimi ndiye Kristo', na watawapotosha wengi.