sw_mat_text_reg/23/29.txt

1 line
326 B
Plaintext

\v 29 Ole wenu, waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mwajenga makaburi ya manabii na kuyapamba makaburi ya wenye haki. \v 30 Ninyi mwasema, kama tungeishi siku za baba zetu, tusingekuwa tumeshiriki pamoja nao kumwaga damu za manabii. \v 31 Kwa hiyo mwajishuhudia wenyewe kwamba ninyi ni watoto wa hao waliowaua manabii.