sw_mat_text_reg/20/25.txt

1 line
441 B
Plaintext

\v 25 Lakini Yesu aliwaita mwenyewe na kuwaambia, "Mnafahamu ya kuwa watawala wa mataifa huwatiisha, na wakuu wao hutekeleza mamlaka juu yao. \v 26 Lakini isiwe hivyo kwenu. Badala yake, yeyote atakayetaka kuwa mkubwa miongoni mwenu lazima awe mtumishi wenu. \v 27 Na atakaye kuwa wa kwanza miongoni mwenu lazima awe mtumishi wenu. \v 28 Kama vile Mwana wa Adamu hakuja kutumikiwa, bali kutumika, na kutoa uhai wake kuwa ukombozi kwa wengi."