sw_mat_text_reg/15/29.txt

1 line
424 B
Plaintext

\v 29 Yesu aliondoka mahali pale na kwenda karibu na bahari ya Galilaya. Kisha alienda juu ya mlima na kuketi huko. \v 30 Kundi kubwa likaja kwake. Na kumletea viwete, vipofu, bubu, vilema na wengine wengi, waliokuwa wagonjwa. Waliwaweka katika miguu ya Yesu na akawaponya. \v 31 Nao umati wakashangaa walipoona mabubu wakiongea, na vilema wakifanywa wazima, viwete wakitembea, na vipofu wakiona. Walimsifu Mungu wa Israeli.