sw_mat_text_reg/15/04.txt

1 line
391 B
Plaintext

\v 4 Kwa kuwa Mungu alisema, 'Mheshimu baba yako na mama yako; na 'Asemaye uovu kwa baba yake na mama yake, hakika atakufa.' \v 5 Lakini ninyi husema, 'Kila amwambiaye baba yake na mama yake, '"Kila msaada ambao angepata kutoka kwangu sasa ni zawadi kutoka kwa Mungu,''' \v 6 "Mtu huyo hana haja ya kumuheshimu baba yake. Katika namna hii mmelitangua neno la Mungu kwa ajili ya mapokeo yenu.