\v 12 Basi Yesu aliposikia kuwa Yohana amekamatwa, aliondoka mpaka Galilaya. \v 13 Aliondoka Nazareti alienda na kuishi Kaperanaumu, iliyoko kandokando na Bahari ya Galilaya, mipakani mwa majimbo ya Zabuloni na Naftali.