sw_mat_text_reg/03/13.txt

1 line
304 B
Plaintext

\v 13 Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka mto Yorodani kubatizwa na Yohana. \v 14 Lakini Yohana alitaka kumzuia akisema, "Mimi nahitaji kubatizwa na wewe, nawe waja kwangu?'' \v 15 Yesu akajibu akasema, ''Ruhusu iwe hivi sasa, kwa kuwa ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote.'' Kisha Yohana akamruhusu.