\v 20 Yesu akawauliza, "Sura na jina hili ni vya nani?" \v 21 Wakamjibu, "Vya Kaisari." Ndipo Yesu akawaambia, "Mpeni Kaisari vitu vilivyo vyake na vya Mungu mpeni Mungu." \v 22 Waliposikia hivyo walishangaa. Kisha walimwacha na kwenda zao.