\v 15 Kama ndugu yako akikukosea, nenda, kamwonyeshe dosari iliyopo kati yako na yeye akiwa pekee yake. Kama akikusikiliza, utakuwa umemrejesha ndugu yako. \v 16 Lakini kama hatakusikiliza, mchukue ndugu mmoja au wawili zaidi pamoja nawe, kwa kuwa kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu kila neno linaweza kuthibitishwa.