\v 22 Lakini Yesu akajibu na kusema, "Haujui kile unachoomba. Je! Unaweza kukinywea kikombe ambacho nitakinywea?" wakamwambia, "Tunaweza." \v 23 Akawaambia, "Kikombe changu hakika mtakinywea. Lakini kukaa mkono wangu wa kulia na mkono wangu wa kushoto si jukumu langu kuwapa, lakini ni kwa wale ambao wamekwisha kuandaliwa na Baba yangu." \v 24 Wanafunzi wengine kumi waliposikia hivyo, wakahuzunishwa sana na wale ndugu wawili.